Tafuta

Vatican News
Simulizi zetu hazina kikomo,zimeandikwa,zinasemwa,zimetengenezwa filam,mlolongo mwingi wa maneno,picha,muziki vile vile na kumbu kumbu ya zamani na maono ya siku zijazo Simulizi zetu hazina kikomo,zimeandikwa,zinasemwa,zimetengenezwa filam,mlolongo mwingi wa maneno,picha,muziki vile vile na kumbu kumbu ya zamani na maono ya siku zijazo 

Dk.Ruffini:haja ya kupata maana ya historia na katika simulizi!

Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano anazungumza na kutafakari kwa kina juu ya Ujumbe wa Papa Francisko kwa ajili ya Siku ya 54 ya Mawasiliano ya duniani ambapo anasisitizia juu umuhimu wa kupata maana ya historia katika kusimulia.

Vatican

Katika machafuko ya sauti na ujumbe unaotuzunguka, tunahitaji hadithi ya kibinadamu, ambazo zinazungumza nasi juu yetu na uzuri ambao unaishi ndani mwetu. Hata tunaposimulia ubaya, tunaweza kujifunza kuanza nafasi ya wokovu, tunaweza kutambua kwa mara nyingine tena katikati ya mabaya hata mwendelezo wa wema na kuupatia nafasi. Katika sentensi hizi moja iliyowekwa mwanzo na sentensi nyingine iliyowekwa karibu na mwisho wa Ujumbe wake kwa ajili ya Siku ya 54 ya Mawasiliano duniani Papa Francisko anatupeleka katika maneno yake kuhusiana na umuhimu wa mada ambayo kwa kipindi imekuwa inatuzunguka. Ni mtazamo wa Dk Paulo Ruffini Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican kuhusu ujumbe wa Papa wa Siku ya Mawasiliano. Bwana Ruffini anasema:  Kama ilivyo kuzunguzungu kinachotaka kutupoteza hewani, mwelekeo, sambamba na hiyo kwamba enzi za mawasiliano ziko hatarini sanjari na ile hatari ya kutowasiliana;  na ushindi wa takwimu  kubwa pamoja na kushindwa kwa hekima lazima ya  kusoma na kusimulia  maana ya kila historia na katika hiyo ndiyo maana ya historia. Kusimulia kunatokana na kufanya uzoefu. Lakini bila kuwa na uwezo wa kupeleka uzoefu katika umoja, hakuna hekima, na hata utambuzi; yote hayo yanaishia katika mlolongo usio na maana.

Kwa maana hiyo inahitaji kusimulia.

Ni kwa njia ya kusimulia tu (daima hata katika sayansi, inahitajika nadharia ya utafiti, ufunguo wa kuelewa mambo) ambapo kuna uwezo wa kuonesha kila ambacho wakati mwingine kwa haraka ni vigumu kuonekana kwa macho, kile ambacho kimejificha, kile ambacho kinahitaji muda wa kutambua ili kuweza kuonekana, anabainisha Dk. Ruffini. Aidha anasema, kwa njia ya Ujumbe wa Papa, anazungumza na watoa habari, kwa uhakika waandishii wa habari; lakini pia kwa watu wote kwa ujumla. Na hii ni kwa sababu wote tunatoa taarifa. Wote tunawajibikaji katika dunia ambayo inafumwa sana na simulizi zetu. Hata hivyo simulizi zetu hazina kikomo, zimeandikwa, zinasemwa, zimetengenezwa filam, mlolongo mwingi wa maneno, picha, muziki; kumbukumbu ya zamani na maono ya siku zijazo, anathibitisha Dk. Ruffini

Simulizi zetu ndiyo maisha ambayo tunarithisha

Papa aanaulizwa kwa watu wote  je  ni hisotria gani ambazo tunasimulia? Tumeziishi kiukweli, tumezitafakari, tumezielewa kabla ya kusimulia? Je ni historia ya kweli?  Je! Ni historia yenye nguvu? Au ni historia ya uwongo? Ni yenye msimamo? Ni historia ambapo ndani mwake kuna mtu na kuna fumbo ambalo linafungwa ndani mwake au ni historia inayomfuta binadamu? Ni historia iliyosimuliwa vizuri au iliyosimuliwa vibaya? Ni historia inayofungulia matumaini au ilifungwa matumaini hayo? Ni historia iyochochea mabaya au inayotafuta kila hali daima zile cheche ya uwezo mzuri wa kuikomboa? Hata hivyp anasema kwa kawaidia historia zote ueleweka mwishoni. Je mwisho wa historia zetu ni upi? Je ni nafasi ipi imewekwakatika fumbo la Mungu, na katika uwezekano wa ukombozi?

Je hekima ya simulizi hiyo iko wapi?

Wenye hekima watu wakubwa wa zamani, anaandika Papa katika Wosia wa Laudato Si, kwamba wangethibitisha juu ya hatari ya kuona hekima yao inakuwa katikati ya kelele na kupotea kwa habari…“Hekima ya kweli, ambayo ni tunda la tafakari, la majadiliano na mkutano wa ukarimu kati ya watu haiwezi  kupatikana katika  wingi wa takwimu na ambazo huishia kueneza na kuwachanganya watu , kama vile  kuona ile aina ya uchafuzi wa akili”.

Siyo mara nyingi tunatambua umuhimu wa nafasi iliyopo ya mawasiliano (na iliyomo ndani ya kila mmoja anapokuwa anawasiliana) ya kuwa zana ya uwelewa au kutoelewana, katika kujenga au katika kuharibu mwamko wenye uwajibikaji, katika kukuza au katika kukuza vibaya utambulisho wetu wa wakati ujao. Aidha Dk Ruffini anasema kutokana na maswali haya, yaani kutoka kwa dhana hii ya uwajibikaji ambayo inatutazama sote, tunaweza kuendelea katika njia hiyo. Na waamini kuichukua kwa mara nyingine tena na ufahamu wa tukio lililobadilisha historia, na kuiangazia fumbo la  Mungu ambaye anakuwa mwanadamu kwa kajili ya  kumkomboa.

Mamajusi waliongozwa na kuelekea njia nyingine ili warudi kwao

Mbele ya fumbo hili, anatumia historia ya Mamajusi walikuwa watu wa hekima  ambao waliweza kuthubutu kupotea, lakini ndiyo hata kama njia ya maisha yetu, ili kuweza kulinda historia ambayo ilikuwa imeoneshwa na Mungu kwa njia ya Mtoto aliyejifanya mwili. Mamajusi walionywa katika ndoto wakati wa kurudi nyumbani il wachague njia nyingine ya kusafiri. Kufuatana na hiyo Dk, Ruffini  anahitimisha kwa kushauri kwamba nasi katika kutafuta nafasi ya kulinda na kupata maana halisi ya historia na kuisimulia ni lazima kuchagua njia nyingine tofauti na ile ambayo imetufikisha hapa leo hii. Katika kuanza upya inahitaji kuanzia na  historia nyingine, namna nyingine ya maono na mtazamo, ya kusimulia, ya kufanya kumbu kumbu, ya kujenga na kisimulia ya wakati endelevu.

28 January 2020, 09:49