Tafuta

Vatican News
Makao ya Mamlaka ya habari za Fedha Vaticann (AIF) Makao ya Mamlaka ya habari za Fedha Vaticann (AIF)  (Vatican Media)

Barbagallo:AIF imerudishwa tena katika kikundi cha Egmont!

Kundi la Egmont limeondoa uamuzi wa kusimamishwa kwa Mamlaka ya habari za Fedha Vatican(AIF) na Rais Barbagallo anasema uamuzi huo unaruhusu kuanza tena kushirikiana na vitengo vya ukaguzi wa kifedha na nchi zingine.

“Ninafurahi kupata habari zilizotolewa na Rais wa Egmont, Mariano Federici, ambaye amenuia kuoandoa uamuzi wa kusimamishwa Mamlaka ya Habari za Fedha (AIF)  kutoka katika mzunguko wa habari kimataifa (“Egmont Secure Web”), uliokuwa umechukua uamuzi huo kunako tarehe 13 Novemba 2019 . Ndivyo alivyo sema Bwana  Carmelo Barbagallo, rais wa Mamlaka ya Habari za Fedha akithibitisha kwamba uamuzi  huo muhimu sana ambao unashuhudia uhakika wa uaminifu uliotolewa  wa usimamizi  wa Egmont dhidi ya mfumo wa habari wa kifedha Vatican.

Sheria zilizo wazi

Aidha Bwana Barbagallo, amesema: “Uamuzi unafuata ufafanuzi uliotolewa na AIF kwa Egmont kuhusu hali ya kipekee ya ukweli uliokuwa unaelezea  kusimamishwa, pamoja na uhakikisho na uslama uliopewa  na AIF kwamba masuala ya habari walizopokea kutoka  katika  mzunguko wa Egmont utakuwa, pia shukrani kwa kusainiwa makubaliano na Msimamizi wa Sheria, sambamba kabisa na sheria zinazosimamia mzunguko huu”.

Uwazi na ushirikiano

Uamuzi huo wa kufuta hatua ya kusimamishwa, unabainisha kuwa,  rais wa AIF, anaruhusiwa kuanza tena kushirikiana na vitengo vya umoja wa ukaguzi wa kifedha wa nchi zingine kwa uwazi kamili na kwa roho ya kushirikiana kabisa.

AIF ni kwa miaka saba inashiriki katika  kikundi cha Egmont

Mnamo Julai 2013, AIF ilikubaliwa katika kujiunga katika Kikundi cha Egmont, ambacho ni jukwaa la ulimwengu linalounganisha kwa pamoja kwa sasa na vitengo vya habari za kifedha kwa nchi 152 na sheria za mamlaka na ambamo sheria za muktadha huo na mazoezi mema ya kushirikiana na kubadilishana habari za kimataifa vinashirikiana. Kufuatia uchunguzi, tangu Mosi Oktoba, Egmont ilikuwa imesimamisha Mamlaka ya Fedha Vatican (AIF) na sasa katika hali ambayo, kama ilivyotangazwa tarehe 23 Januari 2020, imerekebishwa.

23 January 2020, 13:00