Tafuta

Askofu Mkuu Paolo Rudelli ni Balozi wa Kitume nchini Zimbabwe! Askofu Mkuu Paolo Rudelli ni Balozi wa Kitume nchini Zimbabwe! 

Askofu Mkuu Paolo Rudelli ni Balozi wa Kitume nchini Zimbabwe!

Papa Francisko amemteua Askofu Mkuu Paolo RUDELLI kuwa Balozi wa Kitume nchini Zimbabwe.Askofu Mkuu Rudelli alizaliwa huko Gazzaniga (Bergamo)Italia tarehe 16 Julai 1970.

Papa Francisko amemteua Askofu Mkuu Paolo RUDELLI kuwa Balozi wa  Kitume nchini Zimbabwe. Askofu Mkuu Rudelli alizaliwa huko Gazzaniga (Bergamo) Italia tarehe  16 Julai 1970. Alipata daraja la Upadre kunako tarehe 10 Juni 1995 na kuwa masomo ya juu  ya Sheria ya Kanisa na Shahada ya Taalimungu Maadili. Alianza shughuli za kidiplomasia mjini Vatican kunako tarehe 1 Julai 2001.

Katika shughuli zake za kidiplomasita aidha wameza kuwakilisha Vatican katika nchi ya Equador na Poland katika kitengo cha Mahusiano kwenye Ofisi za Katibu Mkuu. Na amekuwa katika Ofisi za Uwakilishi wa Vatican wa Kudumu katika Baraza la Ulaya Strasburg, tangu tarehe 20 Septemba 2014. Askofu Mkuu Rudelli anazungumza lugha 5: kingereza, kifaransa,kispanyola, kipoland na lugha yake ya taifa Kiitaliano.

 

26 January 2020, 14:52