Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko tarehe 9 Desemba 2019 amekutana na kuzungumza na Waziri mkuu wa Slovakia Bwana Peter Pelegrini. Baba Mtakatifu Francisko tarehe 9 Desemba 2019 amekutana na kuzungumza na Waziri mkuu wa Slovakia Bwana Peter Pelegrini. 

Waziri mkuu wa Slovakia akutana na Papa Francisko mjini Vatican

Katika mazungumzo kati ya Baba Mtakatifu Francisko na Bwana Peter Pellegrini, wamegusia kuhusu uhusiano mwema uliopo kati ya nchi hizi mbili na wameonesha nia ya kutaka kuimarisha uhusiano huu wa kidiplomasia kwa kujikita zaidi katika sekta ya elimu. Baadaye, wamejadili pia kuhusu sheria zilizopitishwa hivi karibuni kwa ajili ya kuunga mkono Jumuiya za kidini nchini Slovakia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu, tarehe 9 Desemba 2019 amekutana na kuzungumza na Bwana Peter Pellegrini, Waziri mkuu wa Slovakia, ambaye baadaye amepata pia fursa ya kukutana na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican. Katika mazungumzo kati ya Baba Mtakatifu na Bwana Pellegrini, wamegusia kuhusu uhusiano mwema uliopo kati ya nchi hizi mbili na wameonesha nia ya kutaka kuimarisha uhusiano huu wa kidiplomasia kwa kujikita zaidi katika sekta ya elimu. Baadaye, wamejadili pia kuhusu sheria zilizopitishwa hivi karibuni kwa ajili ya kuunga mkono Jumuiya za kidini nchini Slovakia.

Baba Mtakatifu na Waziri mkuu wa Slovakia wameendelea kujadiliana kuhusu masuala tete kama vile nchi zenye raia wachache, uhuru wa kuabudu na uhuru wa kidini; ukarimu kwa wakimbizi na wahamiaji pamoja na umuhimu wa kudumisha haki jamii. Mwishoni, katika muktadha wa majadiliano yaliyofanywa na Mawaziri wa Mambo ya nchi za nje wa Shirikisho la Ushirikiano wa Kimataifa, Usalama na Maendeleo, OSCE uliofanyika hivi karibuni huko Bratislava chini ya uenyekiti wan chi ya Slovakia. Kimsingi mkutano uligusia changamoto za utunzaji wa mazingira, utawala bora, ulinzi na usalama! Mada za kikanda na kimataifa zimejadiliwa kwa kutoa kipaumbele cha pekee kwa nchi ya Ukraine na nchi zile zilikoko Magharibi mwa Balkan.

Papa: Slovakia
10 December 2019, 16:39