Tafuta

Vatican News
Ndege ya Shirika la Ndege la Kazakhstan, Bek Air imepata ajali na kusababisha zaidi ya watu 12 kupoteza maisha. Ndege ya Shirika la Ndege la Kazakhstan, Bek Air imepata ajali na kusababisha zaidi ya watu 12 kupoteza maisha. 

Ajali ya ndege Kazakhstan, abiria 12 wafariki dunia!

Bek Air, iliyokuwa imebeba abiria 98 kuelekea Nur-Sultan, imepoteza mwelekeo na kuanguka karibu na mji wa Almaty, Ijumaa tarehe 27 Desemba 2019. Taarifa za awali zinasema kwamba, kuna watu zaidi ya 12 ambao wamepoteza maisha. Idadi hii inaweza kuongezeka maradufu. Serikali imeunda tume ili kuchunguza chanzo cha ajali hii. Baba Mtakatifu Francisko ametuma salam za rambi rambi!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Ndege ya Shirika la Ndege la Kazakhstan, Bek Air, iliyokuwa imebeba abiria 98 kuelekea Nur-Sultan, imepoteza mwelekeo na kuanguka karibu na mji wa Almaty, Ijumaa tarehe 27 Desemba 2019. Taarifa za awali zinasema kwamba, kuna watu zaidi ya 12 ambao wamepoteza maisha. Idadi hii inaweza kuongezeka maradufu. Serikali imeunda tume ili kuchunguza chanzo cha ajali hii. Baba Mtakatifu Francisko amepokea taarifa hizi kwa masikitiko makubwa. Katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican anasema, anapenda kutoa salam zake za rambi rambi kwa wote walioguswa na kutikiswa na msiba huu mzito. Baba Mtakatifu anawaombea pumziko la amani, wale wote waliotangulia mbele ya haki na wagonjwa waweze kupata nafuu na hatimaye kupona haraka ili kuendelea na shughuli zao za kila siku. Baba Mtakatifu anapenda kuwatia shime wale wote wanaoendelea kujisadaka kwa ajili ya kuokoa maisha ya abiria wa ndege hii.

Papa: Ajali
27 December 2019, 15:06