Tafuta

Mchana tarehe 31 Desemba 2019 Papa Francisko ameshiriki mazishi ya Profesa Maria Grazia Mara mtaalam wa masomo ya mababa wa Kanisa.Alikuwa na miaka 95 Mchana tarehe 31 Desemba 2019 Papa Francisko ameshiriki mazishi ya Profesa Maria Grazia Mara mtaalam wa masomo ya mababa wa Kanisa.Alikuwa na miaka 95 

Papa ashiriki mazishi ya Maria Grazia Mara mtaalam wa mababa wa Kanisa!

Tarehe 31 Desemba alasiri,Papa Francisko ameshiriki mazishi katika mtindo wa faragha kwa Profesa Maria Grazia Mara, aliyekuwa anafundisha wakati wake katika Taasisi ya Augustinianum. Bi Maria Grazia amefariki tarehe 30 Desemba 2019 akiwa na umri wa miaka 95.Hata hivyo mwaka jana Papa alikuwa amemtembelea katika nyumba yake,Roma.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Mwaka jana Papa Francisko alikuwa amekwenda katika nyumba yake na kushangaza wakazi wa Roma. Amefanya hivyo kwa mara nyingine tena katika safari yake ya mwisho ya buriani. Na  kama rafiki yoyote yule ambaye akiwa kanisani Papa Francisko alikuwa amekaa kwenye viti kama waamni wengine wakati wa ibada ya mazishi.

Profesa Mara alikuwa na miaka 95

Kwa mujibu wa msemaji wa vyombo vya habari Vatican Bwana Matteo Bruni, hili ni tukio la tarehe 3I Desemba alasiri saa 9 ambapo Papa Francisko amekwenda katika Kanisa la Mtakatifu Giuseppe huko Nomentana, Roma kuudhuria mazishi ya Profesa Maria Grazia Mara, aliyekuwa na umri wa miaka 95 na mtaalamu wa masuala ya Mababa wa Kanisa na mwandishi wa vitabu vingi, ambaye kwa hakika ni sura muhimu katika historia ya kikristo.

Ziara ya Papa

Ikumbukwe hata hivyo kuwa ilikuwa ni tarehe 29 Julai 2019 wakati gari la aina Ford Focus ya blu, iliposimama katika makazi na Bi Mara. Kwa kipindi kirefu profesa huyo alikuwa anatamani kumjua Papa Francisko na hakuwa na uwezo huo kwa maana alikuwa ni mgojwa, lakini kwa bahati nzuiri Papa alichagua kwenda kumwona na alikaa kwa muda wa saa moja katika nyumba hiyo  na kurudi tena mjini Vatican.

31 December 2019, 17:16