Tafuta

Papa Francisko asikitishwa na ajali ya ndege ya Kijeshi nchini Chile ambayo imesababisha watu 38 kupoteza maisha. Papa Francisko asikitishwa na ajali ya ndege ya Kijeshi nchini Chile ambayo imesababisha watu 38 kupoteza maisha. 

Papa Francisko asitikishwa na ajali ya ndege nchini Chile, Watu 38 wamefariki dunia

Taarifa ya ajali ya ndege ya Jeshi la Chile, C-130 iliyoanguka tarehe 11 Desemba 2019 na kusababisha watu 38 kupoteza maisha, kati yao wanajeshi wakiwa ni 35 na raia 3 wakati ikielekea huko Antartide. Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa sana na taarifa hii, anawaombea wale wote walioguswa na msiba huu mzito na marehemu wapate rehema kwa Mungu wapumzike kwa amani.

Na Padre Richard A. Mjigwa, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa sana na taarifa ya ajali ya ndege ya Jeshi la Chile, C-130 iliyoanguka siku ya Jumanne tarehe 11 Desemba 2019 na kusababisha watu 38 kupoteza maisha, kati yao wanajeshi wakiwa ni 35 na raia 3 wakati ikielekea huko Antartide. Baba Mtakatifu katika salam za rambi rambi zilizoandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwenda kwa Askofu Santiago Jaime Silva Retamales wa Jimbo la Kijeshi nchini Chile, anapenda kuwahakikishia wananchi wote wa Chile uwepo wake wa karibu hasa kwa wale wote walioguswa na kutiswa na ajali hii mbaya. Anawaombea marehemu wote raha ya milele na mwanga wa milele uweze kuwaangazia na wapumzike wa amani!

12 December 2019, 15:23