Tafuta

Kazi muhimu ni ile ya kutangaza Injili iliyothibitishwa mwaka 2019  kwa njia ya Katekesi zake 41 zilizokuwa zinahusu Sala ya Baba Yetu na Kitabu cha Matendo ya mitume, Sala za Malaika wa Kazi muhimu ni ile ya kutangaza Injili iliyothibitishwa mwaka 2019 kwa njia ya Katekesi zake 41 zilizokuwa zinahusu Sala ya Baba Yetu na Kitabu cha Matendo ya mitume, Sala za Malaika wa  

Papa Francisko kwa 2019:uhakika wa imani na mapambano ya imani kwa Mungy!

Mwaka 2019 umekuwa wa kina kwa Papa Francisko katika safari nyingi na mikutano binafsi kwa lengo moja la kutangaza habari mpya ya huruma ya Mungu.Katekesi 41 kuhusu Sala ya Baba Yetu na Kitabu cha Matendo ya mitume,Sala za Malaika wa Bwana 65 na Malkia wa Mbingu;mahubiri 60 katika maadhimisho kwa umma,mahubiri 44 katika kikanisa cha Mtakatifu Marta na karibia hotuba 260 kwa watu wa Mungu!

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Hata kwa mwaka 2019 Papa Francisko ametuzawadia katekesi rahisi kwa wote juu ya upendo. Kazi muhimu ni ile ya kutangaza Injili iliyothibitishwa   mwaka 2019  kwa njia ya Katekesi zake 41 zilizokuwa zinahusu Sala ya Baba Yetu na Kitabu cha Matendo ya mitume, Sala za Malaika wa Bwana 65 na Malkia wa Mbingu, zaidi ya mahubiri 60 katika maadhimisho kwa umma, mahubiri 44 katika kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican ( bila kuhesabu ujumbe, nyaraka, hati na mahojiano ambayo yamegeuka kuwavitabu vya kujisomea na karibia  hotuba 260 kwa watu wa Mungu.

Uhakika usioleta mchanganyiko

Baba Mtakatifu Francisko kwa wate anawakumbusha kuwa kuishi kwetu daima kuna faraja ya uhakika. Mungu anatupenda na Yesu alitoa maisha yake kwa ajili yetu. Anawaalika kukumbuka kuwa imani rahisi na yenye nguvu ya wakina mama na bibi ambao mara nyingi wamekuwa na wanatoa nguvu na msimamo wa kwenda mbele na bila kuangusha mikono yao, ile imani inayokuwa ndani ya nyumba na ambayo haitambuliki japokuwa, ndiyo ile inayojenga kidogo kidogo Ufalme wa Mungu. Ni imani ambayo haichanganyiki kwa sababu inasisimama juu ya msingi mkuu wa Injili

Imani na kuabudu miungu

Papa Francisko  kwa mwaka mzima anashauri kuabudu Mungu mmoja wa kweli wa Utatu Mtakatifu katika jamii ambayo imekuwa daima ya kipagani. Na kuabudu Miungu anasema siyo lazima kuonekana unakwenda katika hekalu la kipagani na kuabudu sanamu. Hapana kuabudu miungu ni ile tabia ya moyo unapopendelea kufanya jambo kwa sababu, linakuwa kwako rahisi na kumsahamu Bwana.  Miungu imebadilisha jina japokuwa inazidi kuwapo hata sasa anabainisha Baba Mtakatifu. Miungu  hiyo ni fedha, ni kutaka mafanikio, ni kutaka kazi nzuri; ni  kutaka kujitosheleza, kustarahe, na hata miungu yote ambayo inatoa ahadi ya furaha japokuwa  hawezi kamwe kutosheleza na kutoa, badala yake inakuweka kwenye mtego wa utumwa,na  inatuibia upendo! Papa Francisko amethibitisha, Miungu inatoa ahadi ya maisha na kumbe inaondoa maisha hayo, wakati Mungu wa Kweli haombi maisha, badala yake anatoa maisha yake.

Mfalisayo yumo ndani mwetu na hatuachi kujisahihisha 

Maneno ya Papa Francisko mara nyingi ni yenye nguvu sana, na kutafakarisha kwa kina  kama alivyokuwa anajua kufanya hata  Yesu. Hata hivyo Yeye ni Kharifa wake. Kama Yeye anaonya kwa namna ye pekee juu ya tabia ya kifarisaliyo, ambayo hujifanya ni mwenye haki na  kujiona bora zaidi ya wengine. Ni ile dini ya umimi, kwa njia za ibada zake na sala zake. Hata hivyo  Papa anabainisha na kuhoji: Je ni wangapi wanakiri ni wakatoliki na wakati huo huo wamejisahau kuwa wakristo na binadamu zaidi, wamesahahau kutoa ibada ya kweli kwa Mungu ambaye anaonekana kwa njia ya jirani? Papa anatoa pendekezo la kujihukumu binafsi. Na “kwa kila mmoja daima kidogo kuna tabia ya ufarisayo kama vile kiburi na majigambo na ambao kwa hakika ni mabingwa wa kujitetea”. Njia ya kuwa na imani daima ni ile ya kuwa unyenyekevu na kuacha usahihishwe!

Upole dhidi ya mashambulizi

Kama maneno yenye nguvu ya Yesu, hata maneno ya Papa Francisko yanaonesha matokeo ya aina mbili: Kuna haja mbili za kuongoka au kubaki na ugumu zaidi jinsi ulivyo. Na ndipo inaonekana ugumu wa ndani na mashambulizi ya nje. Kwa dhati Papa Francisko haogopi hata kidogo wale wasio amini na wanaondelea  kumshambulia. Vile vile amethibtisha hayo wakati akiwa kwenye ndege ya kurudi jijini Roma kutoka Afrika.   Papa alisema: “ Leo hii tunazo shule nyingi za ugumu ndani ya Kanisa na ambazo siyo wanaokana Mungu japokuwa ni  njia za kikristo kabla ya kumkana Mungu lakini ambao  baadaye wataishia katika njia mbaya kwa sababu nyuma ya tabia hizi za ugumu, hakuna utakatifu wowote wa Injili”.

Kutokana na hiyo Papa Francisko anawaalika kutoa jibu la wema dhidi ya ubaya, ya kuwa wapole mbele ya watu ambao wameshikwa na kishawishi cha kufanya mashambulizi kama hayo kwa sababu wao wako wanapitia matatizo na ambao wanapaswa kusindikizwa kwa upole, alisisitiza. Vile vile watu wengine wanaogopa kuwa Kanisa leo hii siyo Katoliki tena na kusingizia maneno ambayo Papa hajawahi kutamka kamwe katika mdogo wake. Haijawahi kubadilishwa Dogma yoyote, bali kuna hatua moja ya kwenda mbele ambayo ni  ukarimu na  huruma vitu viwili  ambavyo havikufutwa na ibada, lakini kwa kutoa mwaliko mmoja tu wa kuviishi na kufanya uzoefu huo ndani ya moyo!Kuna haja ya kujiuliza je Wakristo wanaweza kweli kuwa na huruma kati yao?

29 December 2019, 11:39