Tafuta

Vatican News
Tarehe 21 Desemba 2019 Papa Francisko  ametia sahini katika Katiba ya kuundwa kwa Kamati ya Wanamajumuyi  majaji kwa ajili ya haki kijamii na mafundisho ya kifransiskani Tarehe 21 Desemba 2019 Papa Francisko ametia sahini katika Katiba ya kuundwa kwa Kamati ya Wanamajumuyi majaji kwa ajili ya haki kijamii na mafundisho ya kifransiskani 

Kuundwa kwa Kamati ya Kudumu ya wanamajumuyi Waamuzi wa Haki kijamii na mafundisho ya kifransiskani!

Kamati mpya ya kudumu ya wanamajumuyi waamuzi wa Haki za kijamii na mafundisho ya kifransiskani imeundwa na majaji wa kike saba kutoka nchi za Afrika kama ifuatavyo:Mina Sougrati (Marocco),Aubierge Oilvia Hungbo-Kploca(Benin),Agatha Anulika Okeke (Nigeria),Hannah Okwengu(Kenya),Jacqueline Rugemalila(Tanzania),Audrey Mashigo(Afrika ya Kusini)na Joyce Kavuma(Uganda).

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Kuanzishwa kwa Kamati ya Kudumu ya Wanamajumuyi ya Waamuzi wa Haki za Jamii na Mafundisho ya Kifransiskani ni moja ya matunda ya Mkutano wa hivi karibuni wa majaji wa kike na waendesha mashtaka kutoka Barani Afrika ulioandaliwa mjini Vatican na Taasisi ya Kipapa ya Sayansi Jamii uliokuwa unahusu  kupambana dhidi ya usafirishaji na uhalifu uliopangwa wa biashara haramu ya watu. Hati ya kuanzishwa kwake imetiwa sahini na Baba Mtakatifu Francisko wakati wa kazi iliyofanyika kunako tarehe 12 na 13 Desemba 2019 huko Casina Pio IV,  Roma.

Kamati hiyo mpya umeundwa na wanamajumuyi majaji wa kike kutoka nchi saba za Afrika kama ifuatavyo:Mina Sougrati (Marocco), Aubierge Oilvia Hungbo-Kploca (Benin), Agatha Anulika Okeke (Nigeria), Hannah Okwengu (Kenya), Jacqueline Rugemalila (Tanzania), Audrey Mashigo (Afrika ya Kusini Sudafrica), na   Joyce Kavuma (Uganda).

Mojawapo ya mipango ya kwanza iliyopangwa katika kiungo kipya ni mkutano wa utakaofikia kilele chake kunako  2020.  Na Kamati ya yake ya Kudumu Wanamajumuyi ya Majaji kwa ajili ya Haki kijamii na Mafundisho ya Kifransiskani, ilianzishwa kunako tarehe 4 Juni 2019. Hilyo ilikuwa ni katika fursa ya Mkutano kwa  ujumla wa mahakimu wa bara la Afrika uliondaliwa mjini Vatican na Taasisi yenyewe ya Kipapa ya Sayansi Jamii ambayo ilikuwa na lengo juu ya  uhusiano kati ya haki za kijamii na mafundisho ya Kifransiskani.

Katika tukio hili Baba Mtakatifu Francisko alizungumza katika hafla hiyo na akapongeza kuanzishwa kwa Kamati ya Kudumu. Mkutano huo ulikuwa umehitimishwa na kusainiwa kwa “Azimio la Roma ambalo lilikuwa linaonesha wazi juu ya wasiwasi ya kuzorota kwa mifumo ya kitaifa na kimataifa kwa namna ya pekee  juu ya uharibifu katika zoezi zima kuhusu haki za kiuchumi, kijamii na kitamaduni.

23 December 2019, 15:16