Tafuta

Vatican News
Katibu wa Baraza la Mawasiliano Vatican Monsinyo Lucio  Adrian Ruiz akisoma Injili ya siku,tarehe 20 Desemba 2019 wakati wa misa ya wafanyazkazi wa baraza hilo iliyoongozwa na Kardinali Comastri Katibu wa Baraza la Mawasiliano Vatican Monsinyo Lucio Adrian Ruiz akisoma Injili ya siku,tarehe 20 Desemba 2019 wakati wa misa ya wafanyazkazi wa baraza hilo iliyoongozwa na Kardinali Comastri  (© Vatican Media)

Kard.Comastri:Kile kinachotufanya kuwa na utofauti ni ukarimu!

Ijumaa subuhi tarehe 20 Desemba 2019 imeadhimishwa misa takatifu kwa wafanyakazi na wahudumu wa Baraza la kipapa la Mawasiliano Vatican.Misa iliongozwa na kwa ajili ya matashi mema ya sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana.Misa hiyo iliongozwa na Kardinali Angelo Comastri,Mhudumu mkuu wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.Wazo kuu la mahubiri ni kuwa na ukarimu kwa kufuata nyayo za watakatifu na watu wenye mapenzi mema.

Katika Misa Takatifu iliadhimishwa kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa kuongozwa na Kardinali Angelo Comastri, Mhudumu mkuu wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican kwa ajili ya wafanyakazi na wahudumu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, Ijumaa subuhi tarehe 20 Desemba 2019. Katika fursa ya kukaribia kusheherekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana, mara baada ya misa hiyo ilifuata afla fupi kwa wafanyakazi wote. Misa imeudhuriwa na wote wafanyakazi, mapadre wakiwemo hata wakuu wa Baraza la Kipapa la Mawasilianoa Bwana Paulo Rufini na Katibu wake Monsinyo Lucio Adrian Ruiz ambaye  alisoma Injili ya siku. Wazo kuu la Kardinali lilikuwa ni kuonesha zaidi utambulisho wa Yesu Kristo kwa mataifa yote, yaani kwa waamini na wasio amini ambapo alitoa mifano kadhaa ya uthibitisho huo. Hata hivyo ametoa maelekezo kwa ajili ya Sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana hasa kwa mkristo wa kweli na kuusisitizia juu ya ukarimu. Akianza mahubiri yake amesema: "Sisi sote tuko sawa kwa Bwana Yesu! awe tajiri au maskini, wenye taaluma  na wasio nayo… Lakini kile kinachotufanya tuwe tofauti ni ule ukarimu. Ki ukweli ni ukarimu tu, unaotufanya tuwe tofauti na  kati ya watu amesisitiza. Kwa maana hiyo ametoa ombi lake kwamba: “Bwana Yesu tufanye angalau tukue ndani mwetu ile chambe chembe ndogo ya ukarimu”. kama vile maneno yaliyomo katika mashairi ya mtunzi wa mashairi wa Italia Umberto Saba (1883-1957).

Mungu alijiunga na upande wa wale walio wapole, wanyenyekvu wenye huruma,

Katika kuitikia ndiyo ni zozezi kubwa la kufanya katika historia nzima ya maisha na ambayo ilipelekea kupiga hatua kubwa na bora na kwa sababu ni katika ndiyo hiyo Mungu aliingia katika familia ya kibinadamu na kusukuma mbele historia ya  kuelekea katika ule ushindi kwa wale walio wema, wapole, wenye huruma, wasafi wa moyo, wahudumu wa amani ambao pia ndiyo watakuwa washindi wa kweli amesisitiza Kardinali Comastri. Hii ni kwa sababu Mungu alijiweka kwenye sehemu hii na kuthibitisha hivyo na ndiyo maana tunaadhimisha Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana, ambayo ni lazima kuifurahia kila mara inapowadia! Karidinali Comastri ameendelea kusema kuwamba  hali hii iliwezesha kutambuliwa hata na watu wengi ambao wako mbali na ukristo kama asemavyo Benedikto wa Msalaba kwamba:“Mimi ni msomi wa historia lakini ninapaswa kutambua kwa hakika  kuwa mambo mapya yaliyojionesha ni katika ukristo”, yaani katika Yesu. Mwingine ni Ghandi mbaye alielezea ya kuwa "heri za mlimani ni kama ncha iliyo ya juu zaidi ya tasaufi ya kikristo!. Vile vile  kama ilivyo kwa mfalsafa Emmanuel Kant aliyefikia kuthibitisha kwamba “Injili ni chemichemi ya ustaarabu wetu wote.”

Yesu anaonekana kwa watakatifu wa nyakati zetu tunaowatambua

 Kardinali Comastri aidha akizidi kufafanua amesema kuwa ujumbe wa Yesu unaonekana hasa katika watakatifu, akianza na Mama Teresa wa Kalcutta ambaye amesema "ni mwanamke maalum wa nyakati zetu ambaye alifungua mkondo wa huruma”. kwa kutoa mfano halisi amesema "Leo hii wanahesabu nyumba 762 zinazo pelekwa mbele huduma ya upendo na Watawa wake, yaani "Wamisionari wa Upendo". Kunako mwaka 1961, amekumbusha Kardinali Comastri kwambwa, Pasolini na Moravia, waliokuwa mbali na imani ya dini, ambapo walikwenda nchini India kuudhuria maadhimisho ya miaka 100tangu kuzaliwa kwa Tagore, lakini pia wakiwa na shauku ya kukutana na mama Teresa. Wa kwanza baada ya kumwona alisema:“haijawahi kutokea roho ya Kristo namna hii iliyo hai na kunivutia kama  a mtawa huyu mdogo na  kwa namna moja au nyingine  mimi kama  kichupukizi angavu ameniwezesha”.  Na katika kifo chake kunako tarehe 5 Septemba 1997,  Indro Montanelli, mwandishi wa habari ambaye pia alikuwa kinyume kabisa na imani ya dini, alisema: “ Ikiwa kila bara lingeweza kuwa na mtu kama mama Teresa, watu wote wasiomjua Mungu wangekwisha duniani”.

Mama Teresa:Tazameni msalaba wa Yesu sisi tunafanya kwa ajili yake 

Kunako mwaka 1973 wakati Mama Teresa alialikuwa kufungua Jumuiya mpya nchini Yemen kwa ajili ya kutibu na kutunza wagonjwa wa ukoma, yeye alikubali kwa haraka. Lakini mara moja alipowasili katika uwanja wa ndege, aliambiwa kutoa msalaba ambao umewekwa juu ya bega katika vazi rasmi la kitawa la Mama Teresa na ndipo yeye alijibu akionesha kwa isahara kuwa: "Tazameni  yote hayo tunayo tenda ni kwa ajili yake. Aidha mnataka tuingie naye wote au hakuna yoyote atakayeingia". Na tangu wakati huo  Kardinali amethibtisha kwamba wameuwawa watawa saba katika nyumba ile ile.

Watakatifu wengine Padre Pio, Yohane XXIII na Mtakatifu Don Bosco

Kardinali Comastri akiendelea na mahubiri yaka vile vile ametaja mtakatifu mwingine wa pili, Padre Pio wa Pietrelcina, ndugu mdogo aliyekuwa mnyenyevu na aliyeishi daima katika kivuli cha konventi, kwa kupokea madonda matakatifu na kuishi nayo kwa miaka hamsini yakiwa yamefunguka na kuwa wazo zaidi kama kioo angavu cha Yesu. Kadhalika mtakatifu wa tatu aliyetajwa ni Mtakatifu Yohane XXIII. Kunako mwaka 1962 katikati ya vita vya kidunia, Meli za kisovieti zilikwenda Cuba zikiwa zimejaza makombora kwa kulenga Amerika. Zilisimama katikati na Papa Yohane XXIII alichukua simu na kuanza kupiga simu kwa usiku mzima huko Washington na Moscow na hatimaye waliweza kweli kukubaliana kati yao amani ikaokolewa! Na hatimaye alitoa mfano mwingine wa nne kama pendekezo la mtindo wa Don Bosco, ambaye alitambua kiukweli tatizo la jamii ya sasa ya kuwa ni elimu. Katika meneno yake, mtakatifu Don Bosco anasema “ ubaya zaidi ya kutibu lazima kuuzuia kwa njia ya kuelimisha vijana".

23 December 2019, 11:40