Tafuta

Baba Mtakatifu Franncisko, tarehe 5 Desemba 2019 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Dr. Igor Zontar, Balozi mpya wa Bosnia na Erzegovina mjini Vatican. Baba Mtakatifu Franncisko, tarehe 5 Desemba 2019 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Dr. Igor Zontar, Balozi mpya wa Bosnia na Erzegovina mjini Vatican. 

Dr. Igor Zontar, awasilisha hati za utambulisho kwa Papa Francisko

Papa Francisko amepokea hati za Utambulisho kutoka kwa Dr. Igor Žontar wa Bosnia na Erzegovina aliyezaliwa kunako tarehe 13 Septemba 1976. Ameoa na kubahatika kupata watoto wawili. Katika maisha yake amebahatika kuwa kufanya kazi katika masuala ya majadiliano ya kidini. Ni mbobezi katika mawasiliano ya kijamii na amebahatika kufanya kazi katika Radio na Majarida ya Kimataifa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa tarehe 5 Desemba 2019 amepokea hati za Utambulisho kutoka kwa Dr. Igor Žontar wa Bosnia na Erzegovina aliyezaliwa kunako tarehe 13 Septemba 1976. Ameoa na kubahatika kupata watoto wawili. Katika maisha yake amebahatika kufanya kazi katika masuala ya majadiliano ya kidini. Ni mbobezi katika mawasiliano ya kijamii na amebahatika kufanya kazi kama Mhariri mkuu wa Jarida na Radio ya Jimbo kuu la Djelo Kriza.

Dr. Igor Žontar ameshiriki katika kuandaa matukio mbali mbali ya kimataifa kwa mfano kunako mwaka 2001 hadi mwaka 2003 aliandaa Mkutano wa Dini Kimataifa. Amewahi kuwa ni mwalimu, mtafiti, mhariri wa Majarida ya Kisayansi Kimataifa. Kuanzia mwaka 2012.2013 alikuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa Radio Maria. Kuanzia mwaka 2015 hadi kuteuliwa kwake, alikuwa ni Jaalimu kwenye Wizara ya elimu nchini Sarayevo.

Papa: Hati za Utambulisho
05 December 2019, 14:47