Baba Mtakatifu Francisko amefikisha miaka 83:matashi mema kutoka dunia nzima!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Huu ni mwezi maalum kwa ajili ya Baba yetu Mtakatifu Francisko, ambaye katika kipindi cha siku chache yaani ilikuwa ni tarehe 13 Desemba ameadhmisha Jubilei ya miaka 50 tangu kupewa daraja la upadre na ambapo Jumanne tarehe 17 Desemba 2019 ametimiza miaka 83 ya maisha yake japokuwapmoa na miaka hiyo haimzuii yeye kuendelea na mbio za kuitanga Injili ya Kristo. Hata hivyo duniani kote, bado wanaendelea kumpongeza sikukuu zake... na kwa mamia elefu ya barua pepe zimefika kutoka kwa waamini wakituma matashi mema katika fura, aidha barua nyingi na michoro yao ya watoto kwa ajili ya Baba Mpendwa Mtakatifu Francisko. Kupitia mitandao ya kimamii, fabook na instagram milioni ya watu wameza kutoa maelezo na maoni yao ya pongezi na sala kwa ajili yake".
Vile vile ujumbe wa barua kutoka kwa viongozi wa dini na serikali kwa matashi mema akianza hata kutoka kwa Baba Mtakatifu Benedikto XVI. Kati ya zawadi zilizopokelewa bila shaka ni jibu la dunia nzima kutokana na yeye anavyozidi kuendelea kuomba wasali kwa ajili ya utume wake katika kiti cha kizamani, kiti cha hekima na ambapo wakati wa Misa Takatifu na Makardinali kunako tarehe 17 Desemba 2016 alikuwa amethibitisha ni kwa jinsi gani yeye ni mwenye utulivu, mwenye furaha na nguvu.
Kwa jina la ubatizo Baba Mtakatifu Francisko anaitwa Jorge Mario Bergoglio aliyezaliwa katika Jiji la Buenos Aires, nchini Argentina nel 1936. Ni mwana wa mhamiaji kutoka mkoa wa Piemonte nchini Italia ambaye pia kwa asili anapenda sana muziki, tangu utoto wake na katika kazi maalum aliweza kuwa anafuatia kwenye radio kila Jumamosi asubuhi akiwa na mama yake Regina na ndugu zake; vile vile katika damu yake anapendelea mpira wa miguuu ijapokua alieleza kuwa akiwa anachaza na marafiki zake, mara nyingi aliishia kuwa mlinda mlango daima!
Alisoma sana na kujifunza kazi mbalimbali, baadaye akapata diploma ya ufundi wa kemia, lakini upeo wa maisha yake ulikuwa ni mwingine. Aliwekwa wakfu kwa Mungu na kujikita katika huduma ya watu hivyo kunako mwaka 1958 aliingia kwenye seminari na kuchagua kuanza unovisi katika Shirika la Mpadre wa Kijesuiti. Katika kipindi hicho ndipo alikutana na nesi mmoja Sr. Cornelia Caraglio, aliy mwokoa maisha yake kwa kumshauri Dk kutumia dozi inayofaa ili kutibu ugonjwa wa pumu. Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba zake mara nyingi amemtumia kama mfano mwema mtawa huyo. Katika mchakato wa kibinadamu na kumbe ulikuwapo tena mpango wa Roho Mtakatifu ambaye alikuwa anamwona baadaye kama Kharifa wa Mtakatifu Petro
Kunako mwaka 1969 alipewa daraja la upadre. Siku hiyo Bbi yake Rosa alimkabidhi barua ikiwalekea wajuuu wake wote ambapo aliyekuwa mdogo ni Jorge Mario, aliyoitunza brua hiyo katika kitabu chake cha sala, ikiwa na maneno yasemayo “ muwe na maisha marefu na yenye furaha. Lakini ikitokea siku moja uchungu, magonjwa au kupoteza mtu mpendwa yupo wa kuwatuliza na kuwapa nguvu na kumbukeni ile pumzi mbele ya Taberkulo, mahali ambapo kuna mfiadini mkumbwa zaidi na mwenye haki; pia mtazame Maria aliye chini ya msalaba ambaye anaweza kuangusha tone la manukato juu ya majeraha ya kina na uchungu”
Kunako mwaka 1973 alitangazwa kuwa mkuu wa Provinsu ya wajesuiti huko Argentina. Kunako mwaka 1992 alichaguliwa kuwa askofu. Na 28 Februari 1998 akatangwa kuwa Askofu Mkuu wa Buenos Aires na kiongozi mkuu wa Kanisa la Argentina. Katika uchaguzi wa tarehe 21 Februari 2001 Mtakatifu Yohane Paulo II alimchagua kuwa Kardinali. Katika fursa hiyo Mtakatifu Paulo II alitamka manenoa haya: " Leo hii asubuhi hii Roma Katoliki inawazunguka makardinali wapya na kuwakumbatia kwa upendo mkuu, kwa utambuzi kuwa wanaandika ukurasa mpya wenye maana katika historia ya maisha yao.
Katika tukio jingine tena muhimu linalokumbwa zaidi ni lile la tarehe 13 Machi 2013 ambapo Kardinali Jorge Mario Bergoglio Askofu Mkuu wa Buenos Aires alichaguliwa kuwa Papa, Mwamerika wa kwanza na Mjesuit wa kwanza, na wakati huo huo Papa wa kwanza kuchagua jina la Francisko kama Mtakatifu wa Assisi ambaye alikuwa na marafiki zake maskini, watu walio wa mwisho, wagonjwa, viumbe vyote vya ardhi, dada Mwezi na kaka Jua na katika moyo wa amani kati ya watu na mataifa. Na ndiyo marafiki hao hao waliompendeza katika maneno ya na ishara za Huduma yake kama Papa! Hongera sana Baba Mtakatifu Francisko katika siku yako ya kuzaliwa!