Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Mheshimiwa Padre Nicolaus Nadji Bab kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Lai nchini Chad. Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Mheshimiwa Padre Nicolaus Nadji Bab kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Lai nchini Chad. 

Padre Nicolas N. Bab ateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Lai, Chad

Askofu mteule Nicolas Nadji Bab alizaliwa tarehe 2 Septemba 1969 huko Bère, Jimbo Katoliki la Laï. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 11 Mei 2002 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu mwaka 2002-2009 alikuwa Paroko na kati ya Mwaka 2009 hadi mwaka 2010 akajiendeleza zaidi kwa masomo huko nchini Hispania. Hadi uteuzi wake alikuwa ni Msimamizi wa Jimbo.

Na Padre Richard A. Mjigwa, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Mheshimiwa sana Padre Nicolas Nadji Bab kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Laï nchini Chad. Askofu mteule Nicolas Nadji Bab alizaliwa tarehe 2 Septemba 1969 huko Bère, Jimbo Katoliki la Laï. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 11 Mei 2002 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu mwaka 2002 hadi mwaka 2009 alikuwa Paroko na kati ya Mwaka 2009 hadi mwaka 2010 akajiendeleza zaidi kwa masomo huko nchini Hispania. Mwaka 2010 akateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki Caritas, Jimbo la Laï. Kati ya Mwaka 2010 hadi mwaka 2018 aliteuwa kuwa Paroko na Msimamizi wa Parokia ya Nodjikwa huko Ngamongo. Kuanzia mwaka 2018 hadi kuteuliwa kwake, alikuwa ni Msimamizi wa Jimbo Katoliki la Laï nchini Chad.

Askofu Chad
14 December 2019, 15:12