Tafuta

Vatican News
Papa Francisko amemteuwa Askofu Stephen Ameyu Martin Mulla kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Juba, Sudan ya Kusini. Papa Francisko amemteuwa Askofu Stephen Ameyu Martin Mulla kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Juba, Sudan ya Kusini.  (Vatican Media)

Askofu Stephen Mulla, ateuliwa kuwa Askofu mkuu wa Juba

Askofu mkuu mteule Stephen A. Martin Mulla, alizaliwa mwaka 1964. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 21 Aprili 1991 akapewa daraja takatifu ya Upadre katika Jimbo Katoliki la Torit Sudan ya Kusini. Tarehe 3 Januari 2019 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Askofu wa jimbo Katoliki la Torit, Sudan Kusini. Askofu mkuu Paulino Loro ameng'atuka kutoka madarakani.

Na Padre Richard A. Mjigwa, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Askofu mkuu Paulino Lukudu Loro, M.C.C.J., wa Jimbo kuu la Juba, nchini Sudan ya Kusini. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Askofu Stephen Ameyu Martin Mulla, kuwa Askofu mkuu mpya wa Jimbo kuu la Juba. Hadi kuteuliwa kwake Askofu mkuu mteule Stephen Ameyu Martin Mulla, alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki laTorit, Sudan ya Kusini. Askofu mkuu mteule Stephen Ameyu Martin Mulla, alizaliwa huko Alodu Jimbo Katoliki la Torit, Sudan Kusini kunako tarehe 10 Januari 1964.

Askofu mkuu mteule Stephen Ameyu Martin Mulla, alijiunga na Seminari ndogo ya Torit, kati ya  mwaka 1978- 1981 na baadaye akaendelea na seminari ya Wau, tangu 1981- 1983. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 21 Aprili 1991, akapewa daraja takatifu ya Upadre katika Jimbo katoliki  la Torit Sudan ya Kusini. Tarehe 3 Januari 2019 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Askofu wa jimbo Katoliki la Torit, Sudan Kusini. Katika maisha na utume wake amewahi kuwa: Jaalim na Profesa na Dekano wa wa Seminari Kuu ya Mtakatifu Paulo, Jimbo kuu la Juba, Sudan ya Kusini.

12 December 2019, 15:05