Askofu mkuu Luigi Ventura aliyekuwa Balozi wa Vatican ameng'atuka kutoka madarakani. Askofu mkuu Luigi Ventura aliyekuwa Balozi wa Vatican ameng'atuka kutoka madarakani. 

Askofu mkuu Luigi Ventura ang'atuka kutoka madarakani

Askofu mkuu Luigi Ventura mwenye umri wa miaka 75 ambaye alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Ufaransa. Hii ni fursa ya kuweza kushughulikia kikamilifu kesi ya kashfa ya nyanyaso za kijinsia inayomwandama kwa wakati huu. Tangu mwaka 2009 amekuwa ni Balozi wa Vatican nchini Ufaransa. Nafasi yake inasimamiwa na Monsinyo Andrea Ferrante, mshauri wa kwanza Ubalozini hapo.

Na Padre Richard A. Mjigwa, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la kutaka kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Askofu mkuu Luigi Ventura mwenye umri wa miaka 75 ambaye alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Ufaransa. Hii ni fursa pia ya kuweza kushughulikia kikamilifu kesi ya kashfa ya nyanyaso za kijinsia inayomwandama kwa wakati huu. Tangu mwaka 2009 amekuwa ni Balozi wa Vatican nchini Ufaransa. Kwa sasa nafasi yake inasimamiwa na Monsinyo Andrea Ferrante, mshauri wa kwanza Ubalozini hapo.

Serikali nchini Ufaransa ina mshutumu Askofu mkuu Ventura kwa kujihusisha na vitendo vya nyanyaso za kijinsia katika matukio makuu manne. Mwezi Julai, 2019, Vatican ilimwondolea Askofu mkuu Luigi Ventura kinga ya kidplomasia na kwamba, Vatican tangu wakati huo imeonesha nia ya kutaka kushirikiana na vyombo vya sheria nchini Ufaransa ili kuhakikisha kwamba, ukweli unafahamika na haki inatendeka kwa wahusika wote!

Ufaransa
18 December 2019, 10:45