Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Gabriel Sayaogo kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu Koupèla, Burkina Faso. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Gabriel Sayaogo kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu Koupèla, Burkina Faso. 

Askofu Gabriel Sayaogo ateuliwa kuwa Askofu mkuu Koupèla, B.Faso

Askofu mkuu mteule Gabriel Sayaogo alizaliwa tarehe 7 Januari 1962 huko Niessega, Burkina Faso. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 13 Julai 1991 akapewa daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 28 Desemba 2010, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu na hatimaye, kuwekwa wakfu kama Askofu hapo tarehe 30 Aprili 2011.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la kutaka kung’atuka kutoka madarakani lililowasikilishwa kwake na Askofu mkuu Séraphin François Rouamba wa Jimbo kuu Jimbo la Koupéla nchini Burkina Faso. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteuwa Askofu Gabriel Sayaogo kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Koupéla lililoko nchini Burkina Faso. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu mteule Gabriel Sayaogo alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Manga, Burkina Faso.

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Gabriel Sayaogo alizaliwa tarehe 7 Januari 1962 huko Niessega, Burkina Faso. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 13 Julai 1991 akapewa daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 28 Desemba 2010, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu na hatimaye, kuwekwa wakfu kama Askofu hapo tarehe 30 Aprili 2011.

Burkina Faso

 

 

07 December 2019, 16:25