Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la Askofu Emmanuel Bushu la kutaka kung'atuka kutoka madarakani. Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la Askofu Emmanuel Bushu la kutaka kung'atuka kutoka madarakani. 

Askofu Emmanuel Bushu wa Jimbo la Buèa ang'atuka kutoka madarakani

Askofu mstaafu Emmanuel Bushu wa Jimbo Katoliki Buéa alizaliwa tarehe 31 Julai 1944. Kumbe, ameng’atuka kutoka madarakani akiwa na umri wa takribani miaka 75. Alipadrishwa kunako tarehe 7 Januari 1973 kumbe, amelitumikia Kanisa kama Padre kwa miaka 46 na ushee! Amewafundisha, kuwaongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu kama Askofu kwa muda wa miaka 26!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu Emmanuel Bushu wa Jimbo Katoliki Buéa, nchini Cameroon la kutaka kung’atuka kutoka madarakani.  Itakumbukwa kwamba, Askofu mstaafu Emmanuel Bushu wa Jimbo Katoliki Buéa alizaliwa tarehe 31 Julai 1944. Kumbe, ameng’atuka kutoka madarakani akiwa na umri wa takribani miaka 75. Alipadrishwa kunako tarehe 7 Januari 1973 kumbe, amelitumikia Kanisa kama Padre kwa miaka 46 na ushee! Mtakatifu Yohane Paulo II alimteuwa kuwa Askofu tarehe 17 Desemba 1992 na kusimikwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Yagoua nchini Cameroon. Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kunako tarehe 3° Novemba 2006 akamteua kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Buéa, nchini Cameroon na kusimikwa rasmi hapo tarehe 30 Januari 2007. Katika muktadha huu, amewafundisha, kuwaongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu kwa takribani miaka 26 kama Askofu. Tarehe 28 Desemba 2019 ameng’atuka kutoka madarakani!

Cameroon
28 December 2019, 14:27