Papa Francisko amemteuwa Mheshimiwa Padre Daniel Nzika kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Impfondo nchini Congo Brazzaville. Papa Francisko amemteuwa Mheshimiwa Padre Daniel Nzika kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Impfondo nchini Congo Brazzaville. 

Padre Daniel Nzika ateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Impfondo

Askofu mteule Daniel Nzika alizaliwa tarehe 16 Februari 1971. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 9 Desemba 2000 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo, amewahi kuwa Paroko usu, Paroko na Mlezi wa maisha ya kiroho; Paroko na hatimaye, Makamu wa Askofu kuanzia mwaka 2010 hadi mwaka 2012. Kuanzia mwaka 2012 hadi mwaka 2015.

Na Padre Richard A. Mjigwa, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la kutaka kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Askofu Jean Gardin, C.S.Sp wa Jimbo Katoliki la Impfondo, lililoko nchini Congo Brazzaville. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Mheshimiwa sana Padre Daniel Nzika kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Impfondo. Askofu mteule Daniel Nzika alizaliwa tarehe 16 Februari 1971. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 9 Desemba 2000 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo, amewahi kuwa Paroko usu, Paroko na Mlezi wa maisha ya kiroho; Paroko na hatimaye, Makamu wa Askofu kuanzia mwaka 2010 hadi mwaka 2012. Kuanzia mwaka 2012 hadi mwaka 2015 alijiendeleza kwa masomo na hatimaye kujipatia shahada ya uzamili katika taalimungu sadikifu. Na kati ya mwaka 2016 hadi kuteuliwa kwake kuwa Askofu, ameendelea kuwa ni Makamu Askofu Jimbo Katoliki la Impfondo.

12 December 2019, 14:22