Mheshimiwa Padre Augustine Ndebueze Echema ameteuliwa kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Aba, nchini Nigeria. Mheshimiwa Padre Augustine Ndebueze Echema ameteuliwa kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Aba, nchini Nigeria. 

Mh. Padre Augustine Ndubueze ateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Aba, Nigeria

Askofu mteule Augustine Ndubueze Echema alizaliwa tarehe 28 Desemba 1958 Jimboni Aba. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 16 Agosti 1986 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo, amewahi kuwa mwalimu na mlezi wa Seminari Ndogo ya “St. Peter Claver” huko Okpala na Paroko. Kwa miaka kadhaa amekuwa ni mshauri kwa waamini walei!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Augustine Ndubueze Echema kutoka Jimbo Katoliki la Owerri kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Aba, nchini Nigeria. Hadi kuteuliwa kwake, Askofu mteule Augustine Ndubueze Echema alikuwa ni Jaalimu wa Liturujia katika Taasisi ya “The Catholic Institute of West Africa (CIWA) iliyoko mjini Port Harcourt. Askofu mteule Augustine Ndubueze Echema alizaliwa tarehe 28 Desemba 1958 Jimboni Aba. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 16 Agosti 1986 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo, amewahi kuwa mwalimu na mlezi wa Seminari Ndogo ya “St. Peter Claver” huko Okpala na Paroko.

Kati ya Mwaka 1989 hadi mwaka 1994 alipelekwa na Jimbo kujiendeleza zaidi katika masomo ya Liturujia na kujipatia Shahada ya Uzamivu katika Liturujia kutoka Chuo Kikuu cha “Philosophisch-Theologische Hochschule Sankt Georgen”, Ujerumani. Baadaye kwa muda wa mwaka mmoja, yaani kati ya mwaka 1994 hadi mwaka 1995 aliteuliwa kuwa Paroko wa Parokia ya “St. Joseph huko Schwalbach,  Jimbo Katoliki la Limburg, nchini Ujerumani. Kati ya mwaka 1996-1998 amekuwa ni Padre mshauri mwambata kwenye Taasisi ya“The Catholic Institute of West Africa (CIWA) iliyoko mjini Port Harcourt. Tangu mwaka 1996 amekuwa ni Jaalimu wa Liturujia kwenye Taasisi hii pamoja na kuwa ni Mwenyekiti wa Tume ya Liturujia Jimbo Katoliki la Owerri. Alikuwa pia ni Mshauri wa maisha ya kiroho wa Baraza la Waamini Walei Kanda ya Owerri.

Jimbo la Aba Nigeria
28 December 2019, 14:43