Wakimbizi na wahamiaji wanaokimbia mateso wanapaswa wakaribishwe,walindwe,wasaidiwe na kushirikishwa kwa mujibu wa Askofu Mkuu Auza Mwakilishi wa Vatican katika UN Wakimbizi na wahamiaji wanaokimbia mateso wanapaswa wakaribishwe,walindwe,wasaidiwe na kushirikishwa kwa mujibu wa Askofu Mkuu Auza Mwakilishi wa Vatican katika UN 

Vatican:Zinahitajika jitihada za pamoja ili kuuondoa uhalifu katika kurasa za historia!

Katika kikao cha 74 cha Umoja wa Mataifa,huko New York,Marekani,Askofu Mkuu Bernardito Auza katika hotuba yake amejikita kuhusu sheria za kimataifa na juu ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.Lazima kuhukumu wahalifu dhidi ya ubinadamu na zaidi kuhamasisha jitihada kwa ngazi zote ili kuuondoa uhalifu kama huo katika kurasa za kihistoria.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Askofu Mkuu Bernardito Auza, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Kikao cha 74 cha Umoja wa Mataifa hivi karibuni mjini New York Marekani wakati wa hotuba yake amegusia sheria na haki za kimataifa na juu ya uhalifu dhidi ya ubinadamu. Katika hotuba yake anasema:ni sababu kubwa ya wasiwasi katika dunia hii inayoendelea na kutishiwa vurugu na ghasia za kisiasa, kidini na kikabila. Ni hali halisi na iliyopo kwa walio wengi ambao wanaogopa kunyongwa, kuuwawa, kufanywa watumwa, kubakwa, kufukuzwa makwao au kuuzwa kwa sababu wao wanashiriki kuwa sehemu ya siasa, dini na kabila. Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Auza anasema, ni lazima kuhukumiwa wahalifu dhidi ya ubinadamu na muhimu zaidi kuhamasisha jitihada kwa ngazi zote ili kuhukumu na kuondoa uhalifu kama huo katika kurasa za kihistoria.

Wahamiaji na wakimbizi

Askofu Mkuu Auza pia katika hotuba yake anaunga mkono kwa kazi inayofanywa ya ushirikiano wa maendeleo ya mkataba wa kimataifa. Na katika kuchunguza maandishi yaliyopendekezwa na Tume ya sheria za kimataifa, anasema inapaswa kwa namna ya pekee kukubali kwa dhati juu ya rasimu ya Ibara ya 5 inayohusu kanuni ya kutowarudisha wakimbizi na wahamiaji. "Hakuna mtu yoyote anapaswa arudishwe mahali ambapo  ametoka kwani anaweza akawa mwathirika wa uhalifu dhidi ya ubinadamu. Wakimbizi na wahamiaji wanaokimbia mateso wanapaswa wakaribishwe, walindwe, wasaidiwe na kushirikishwa".

Ushirikiano wa kimataifa

Hata hivyo Askofu Mkuu Auza katika hotuba hiyo ameweza kuelekeza kwa ushirikiano wa kimatafa njia mwafaka ya kupambana na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Kwa mujibu wake, anatoa vipaumbele viwili ambavyo vinatakiwa kuzingatiwa hasa vilivyopo katika ushirikishwaji wa mkataba wa Kimataifa. Anasema awali ya yote Mkataba huo mpya unapaswa kuwapa raia wote fursa ya kutafuta haki na kufanya isikike sauti zao kwa ngazi ya kimataifa. Na kipaumbele cha pili ambacho anaelekeza  hatimaye ni mkataba wa siku sijazo ambao  anathibitisha kwamba ni lazima uweze kuwa na maono ya mbele ya hitaji la kusaidia Mataifa na mifumo dhaifu ya kisheria.

04 November 2019, 14:05