Baba Mtakatifu Frsancisko tarehe 8 Novemba 2019 amekutana na kuzungumza na Rais Gitanas Nausèda wa Lithuania. Baba Mtakatifu Frsancisko tarehe 8 Novemba 2019 amekutana na kuzungumza na Rais Gitanas Nausèda wa Lithuania. 

Rais Gitanas Nausèda akutana na Papa Francisko mjini Vatican

Katika mazungumzo yao ya faragha, viongozi hawa wamegusia kuhusu: Mchango wa Kanisa katika ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini Lithuania. Wameangalia pia changamoto, matatizo na fursa zilizoko nchini Lithuania mintarafu masuala ya kiuchumi na kijamii pamoja na umuhimu wa kukuza na kudumisha tunu msingi za maisha ya ndoa na familia, ukarimu na haki jamii.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 8 Novemba 2019 amekutana na kuzungumza na Rais Gitanas Nausèda wa Lithuania ambaye, baadaye amekutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican. Katika mazungumzo yao ya faragha, viongozi hawa wawili wamegusia kuhusu mchango wa Kanisa katika ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini Lithuania. Wameangalia pia changamoto, matatizo na fursa zilizoko nchini Lithuania mintarafu masuala ya kiuchumi na kijamii.

Baadaye, Baba Mtakatifu pamoja na mgeni wake, wamezungumzia kuhusu: umuhimu wa kukuza na kudumisha tunu msingi za maisha ya ndoa na familia, ukarimu na haki jamii. Mwishoni, Baba Mtakatifu na Rais Gitanas Nausèda wa Lithuania, katika mazungumzo yao, wamerejea katika masuala ya kikanda na kimataifa, hasa kuhusiana na masuala ya amani na usalama; mgogoro wa kisiasa nchini Lithuania pamoja na umuhimu wa Jumuiya ya Kimataifa kujikita katika mchakato wa ujenzi wa mshikamano wa kimataifa hususan Barani za Ulaya, ili kukabiliana na changamoto mamboleo zinazoendelea kujitokeza Barani Ulaya.

Papa: Lithuania

 

08 November 2019, 14:52