Tafuta

Vatican News
Dr. Renè Bruelhart amemaliza muda wake kama Rais wa Baraza la Mamlaka ya Habari za Kifedha Vatican na kupongezwa na Papa Francisko. Dr. Renè Bruelhart amemaliza muda wake kama Rais wa Baraza la Mamlaka ya Habari za Kifedha Vatican na kupongezwa na Papa Francisko. 

Dr. Renè Bruelhart amemaliza muda wake kama Rais wa AIF.

Dr. René Brüelhart, Rais wa Baraza la Mamlaka ya Habari za Kifedha Vatican, AIF, amemaliza muda wake. Papa Francisko amempatia dhamana ya kumtafuta mtu mwaminifu, mwenye weledi, mwadilifu na anayetambulikana kimataifa atakayechukua nafasi yake, mtu huyo atatangazwa mara tu baada ya kurejea mjini Vatican kutoka kwenye hija yake ya kitume nchini Thailand na Japan.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemshukuru na kumpongeza Dr. René Brüelhart, Rais wa Baraza la Mamlaka ya Habari za Kifedha Vatican, AIF, aliyemaliza muda wake na kumsihi atafute mtu mwaminifu, mwenye weledi, mwadilifu na anayetambulikana kimataifa atakayechukua nafasi yake. Baba Mtakatifu anasema, atamtangaza mtu huyo atakayekuwa amempendekeza mara tu baada ya kurejea mjini Vatican kutoka kwenye hija yake ya kitume nchini Thailand na Japan kuanzia tarehe 19 hadi 26 Novemba 2019. Wakati huo huo Baraza la Mamlaka ya Habari za Kifedha Vatican, AIF, litaendelea kutekeleza shughuli zake za ndani na zile za kimataifa.

Papa: AIF
18 November 2019, 14:11