Tafuta

Vatican News
Papa Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Paulin Batairwa Kubuya kuwa Katibu mkuu msaidizi, Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini. Papa Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Paulin Batairwa Kubuya kuwa Katibu mkuu msaidizi, Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini.  (Vatican Media)

Padre Paulin Batairwa Kubuya ateuliwa kuwa Katibu mkuu msaidizi majadiliano ya kidini

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Paulin Batairwa Kubuya, S.X, kuwa Katibu mkuu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini. Kabla ya uteuzi huu, Padre Paulin Batairwa Kubuya alikuwa ni Katibu mtendaji, Tume ya Majadiliano ya Kidini na Kiekumene ya Baraza la Maaskofu Katoliki Mkoa wa Taiwan na Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Fu Jen.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Paulin Batairwa Kubuya, S.X, kuwa Katibu mkuu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini. Kabla ya uteuzi huu, Padre Paulin Batairwa Kubuya alikuwa ni Katibu mtendaji, Tume ya Majadiliano ya Kidini na Kiekumene ya Baraza la Maaskofu Katoliki Mkoa wa Taiwan. Pamoja na shughuli hizi, alikuwa pia ni Mhadhiri Mwandamizi wa masuala ya kidini Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Fu Jen.

Katibu Msaidizi
12 November 2019, 11:48