Tafuta

Mti utakaopambwa mjini Vatican  kwa ajili ya sherehe za Kuzaliwa kwa Bwana utakuwa na urefu wa mita 26 pia pango litakalo tengenezwa vitazinduliwa rasmi tarehe 5 Desemba 2019 Mti utakaopambwa mjini Vatican kwa ajili ya sherehe za Kuzaliwa kwa Bwana utakuwa na urefu wa mita 26 pia pango litakalo tengenezwa vitazinduliwa rasmi tarehe 5 Desemba 2019 

Mti wa urefu wa mita 26 utapambwa kwa ajili ya siku kuu ya Kuzaliwa Bwana

Mti mrefu wa kuweza kupambwa kwa ajili ya sikukuu za kuzaliwa kwa Bwana mwaka huu umeletwa kutoka katika wilaya ya Trento,Italia ambao ni wenye urefu wa mita 26.Tarehe 5 Desemba kutakuwapo na uzinduzi wa Pango pia kuwashwa kwa taa kwa mti huo kwenye uwanja wa Mtakatifu Petro saa 10.30 za jioni masaa ya Ulaya.

Mti wa kuweza kupambwa kwa ajili ya Sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana, wenye urefu wa mita 26 kwa mwaka huu unatokea eneo la Asiago huko Trentino nchini Italia ambao utakuwa mjini Vatican kwa kipindi chote cha maadhimisho ya sikikuu ya Kuzaliwa kwa Bwana. Pango na mti  huo vimetolewa kwa mwaka huu kutoka katika maneo hayo kufuatia na kukumbusha juu ya kimbunga kikali kilichotekea mwezi Oktoba–Novemba 2018 na kukumba maeneo ya Triveneto nchi ni Italia.

Wasanii kutoka Conegliano na Scurelle 

Upambaji na utengenezaji wa Pango vitakuwa tayari  kufikia tarehe 5 Desemba 2019 katika uwanja wa Mtakatifu Petro na ambapo siku hiyo vitazinduliwa na kubaki hadi  tarehe 12 Januari 2019, baada ya kumaliza sikukuu hizo. Hata hivyo mti mrefu huo umetolewa zawadi na baadhi ya miti mingine kama 20 iliyo midogo kutoka katika eneo la Rotzo-Pedescala na Mtakatifu  Pietro wilayani Vicenza Italia. Hata hivyo mwaka huu Kikundi cha Wasanii wa kutengeneza mapango kiitwacho Parè cha Conegliano, wilaya ya Treviso kitafanya hata maandalizi ya kupamba pango ndani ya Ukumbi wa Paulo VI.

Tarehe 5 Desemba ni uzinduzi rasmi wa pango na mti uliopambwa

Tarehe 5 Desemba 2019 kutakuwapo na uzinduzi wa Pango na kuwashwa kwa taa katika mti wa Noeli kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro saa 10.30 za jioni masaa ya Ulaya. Afla hiyo itaongozwa na Kardinali Giuseppe Bertello, na askofu Fernando Vérgez Alzaga, wote wawili akiwa ni Rais na katibu wa Mamlaka ya Serikali ya mji wa Vatican. Taarifa zinasema kwamba, asubuhi ya siku hiyo tarehe 5 Desemba wawakilishi wa kutengeneza pango kutoka Scurelle na wa Mtakatifu Pietro Piacenza na kikundi cha wasanii cha Parè ya Conegliano watakutana na Baba Mtakatifu Francisko kwa uwakilishaji maalum wa zawadi.

16 November 2019, 15:03