Vatican News
Baba Mtakatifu amemteua Askofu  Gabriele Giordano Caccia kuwa Mwakilishiw a Kudumu katika Ofisi za Umoja wa Mataifa New York Baba Mtakatifu amemteua Askofu Gabriele Giordano Caccia kuwa Mwakilishiw a Kudumu katika Ofisi za Umoja wa Mataifa New York 

Askofu Mkuu Caccia ni Mwakilishi mpya wa Kudumu katika Ofisi za Umoja wa Mataifa!

Baba Mtakatifu Francisko alimteua Askofu mkuu Caccia kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa.Ni mwenye umri wa miaka 61 mzaliwa wa Milano nchini Italia.Hadi uteuzi wake alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Ufilippini.

Askofu Gabriele Giordano Caccia, mwenye umri wa miaka 61 mzaliwa wa Milano nchini Italia  ndiyo mwakilishi mpya wa kudumu wa Vatican katika ofisi za Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani. Hadi sasa nafasi hiyo ilikuwa inafunikwa na Askofu Mkuu Bernardito Auza. Askofu Gabriele Giordano Caccia ni Askofu Mkuu katika Jimbo la Sepino,na Balozi wa Vatican nchini Filippine kuanzia mwaka 2017.

Askofu Mkuu Caccia alizawalia Milano tarehe 24 Februari 1958 na akapewa daraja la upadre na Kardinali Carlo Maria Martini, tarehe 11 Juni 1983 na kuendelea na shughuli za kichungaji  kiparokia hadi  1986. Baadaye alikwenda kwenya mafunzo zaidi akiwa katikaTaasisi ya Kipapa ya Roma na kupata shahada ya udaktari wa Taalimungu na Sheria katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana.

Alianza shughuli za kidiplomasia mjini Vatican kunako tarehe 1 Julai 1991 na kuwa mwakilishi katika ofisi ya ubalozi wa Vatican nchini Tanzania. Tarehe Mosi, Juni 1993 aliitwa tena ili kuendelea na shughuli yake katika Kitengo cha Sekretarieti kuu ya Vatican katika kitengo cha Katibu Mkuu msaidizi wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa. Tarehe 17 Desemba 2002 akateuliwa kuwa mshauri katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa  Mambo ya nchi za Nje na ushirikiano wa kimataifa.

Tarehe 16 Julai 2009 aliteuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Lebanon na kupewa Kanisa la Sepino. Na tangu 2017 aliteuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Filippine  Aliwekwa wakfu kuwa Askofu mkuu kwa njia ya mikono ya Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI, kunako tarehe 12 Septemba 2009 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

16 November 2019, 14:42