Tafuta

Vatican News
Kujitoa kwa Mungu ni tendo la ukuu wake katika kumfuasa mwanaye aliyejitoa sadaka kwa ajili ya watu wote Kujitoa kwa Mungu ni tendo la ukuu wake katika kumfuasa mwanaye aliyejitoa sadaka kwa ajili ya watu wote 

Mhs.Padre Joseph Kizito ni Askofu mpya wa Jimbo la Aliwal-Afrika Kusini!

Tarehe 15 Novemba 2019 Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Joseph Kizito kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Aliwal,Afrika ya Kusini.Hadi uteuzi wake alikuwa ni makamu Askofu wa Jimbo hilo hilo.Alizaliwa kunako mwaka 1967 Kampala Uganda.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu wa Jimbo Katoliki la  Aliwal, Afrika ya Kusini Mheshimiwa Padre  Joseph Kizito  wa jimbo hilo hilo, ambaye hadi uteuzi wake alikuwa ni Makamu Askofu na Paroko wa Aliwal. Mheshimiwa Padre Joseph Kizito alizaliwa tareh 2 Julai 1967 Kampala Uganda. Alisomea mafunzo ya Falsafa katika Seminarti Kuu ya Mtakatiufu Augustine (Lesotho), Taalimungu katika Seminari ya Mtakatifu John Vianney, Pretoria, Afrika Kusini. Alipewa daraja la upadre kunako tarehe 27 Septemba 1997 na kuwekwa katika Jimbo Katoliki Aliwal, Afrika Kusini.

Shughuli za utume wake Padre Mteule

Katika shughuli zake za kitume ni  kuanzia 1997-1998 amekuwa Paroko msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu Francis Xavier; 1998-2003 kuwa Parokia ya Mtakatifu Augustine huko Dordrecht; 2003-2013 kuwa katika Paroko wa Parokia ya Sterkspruit; Tangu 2008 amekuwa Makamu wa Askofu katika  Jimbo Katoliki Aliwal; na tangu  2013 ni Paroko wa Kanisa Kuu la Aliwal.

15 November 2019, 12:15