tarehe 24 Novemba 2019 kimetangazwa Kikundi kipya cha vijana washauri kimataifa cha Baraza la Kipapa la Walei,Familia na Maisha. tarehe 24 Novemba 2019 kimetangazwa Kikundi kipya cha vijana washauri kimataifa cha Baraza la Kipapa la Walei,Familia na Maisha. 

Kikundi cha vijana washauri kimataifa kimeundwa!

Katika Sikukuu ya Kristo Mfalme,Baraza la Kipapa,Walei Familia na maisha wametangaza kwa furaha kuanzishwa kiungo cha ushauri kimataifa cha vijana,chenye wajumbe 20 kutoka kanda tofauti za dunia na baadhi ya vyama na mashirika ya kitume na jumuiya za kimataifa.Hii ni kwa mujibu wa utekelezaji wa ombi la hati ya mwisho ya Sinodi ya 2018 ya kuweka kiungo cha kuwakilisha vijana kwa ngazi ya kimataifa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika Hati ya mwisho ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili a vijana 2018 kulikuwapo na kipengele ambacho kilikuwa kinahusu jitihada za kuongeza nguvu katika shughuli za Ofisi ya Vijana  hasa kwa upande wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha ambalo kwa njia ya Katiba yake “kuweka kiungo cha kuwakilisha vijana kwa ngazi ya kimataifa” (n. 123). Katika msimamo huo Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha hatimaye katika Sikukuu ya Kristo Mfalme Jumapili tarehe 24 Novemba 2019 wameunda kiungo cha ushauri kimataifa cha  vijana, kwa kuwatangaz  vijana wajumbe washauri 20 kutoka katika kanda tofauti za dunia na baadhi ya vyama, mashirika  katoliki na jumuiya za kimataifa, ambao watakuwapo katika kiungo hicho kwa miaka mitatu. Hawa ni vijana ambao wamehusishwa katika michakato mbali mbali na zaidi  ya Sinodi kwa mfano katika Jukwaa la Kimataifa, lililo andaliwa na Baraza  la Kipapa la Familia mwezi Juni mwaka huu ili kuhamasisha matendo hai ya Wosia wa Kitume wa Christus vivit.

Shughuli za vijana washauri kimataifa

Kikundi cha vijana 20 kilichoteuliwa na kutangazwa kitafanya utume wake muhimu wa kushauri na kutoa mapendekezo, kushirikiana na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha kwa kujikita kwa kina juu ya masuala yanayohusu maisha ya kichungaji kwa vijana, hata baadhi ya matinki msingi kwa ujumla yanayo stahili kama vile Wosia wa Christus vivit. Hata hivyo Mkutano wa kwanza wa kikundi hiki unatarajiwa kuwafanyika mjini Roma mwezi Aprili 2020.

Vijana hawa wanatoka sehemu mbali mbali za dunia

Majina ya vijana hao na wanapotokea ni kama ivyatavyo:  Béatrice CAMARA (Guinea), Moses OJOK (Uganda), Dominique YON (Afrika Kusini), Brenda NORIEGA (Marekani), Joseph Edward SAN JOSE (Canada), Sofía Beatriz CRUZ ESTRADA (El Salvador), Natalia GARCÍA JIMÉNEZ (Porto Rico), Ariel Alejandro ROJAS HERNÁNDEZ (Chile), Agatha Lydia NATANIA (Indonesia), Jesvita Princy QUADRAS (India), Makoto YAMADA (Japan ), Tilen ČEBULJ (Slovenia), Chiara VAN VOORST (Nchi za Ulaya Mashariki), Émile ABOU CHAAR (Lebanon), Ashleigh GREEN (Australia), Carina BAUMGARTNER ( Austria), Lucas Ricardo MARÇAL RAMOS (Brazil), Lucas PETIT NAVARRO (Ufaransa), Tommaso SERENI (Italia), Tomás VIRTUOSO (Ureno). Kwa maelezo zaidi unaweza  kujisomea kupitia: http://www.laityfamilylife.va/content/laityfamilylife/en/news/2019/istituzione-dellorganismo-consultivo-internazionale-dei-giovani.html

Ujumbe wa Mkutano wa kitaifa kwa wakala wa kichungaji wa Familia na maisha  nchini Guatemala

Wazee ni tunu msingi kwa ajili ya familia, na familia ni tunu kwa ajili ya wazee, ndiyo ujumbe wa Katibu Mkuu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha Bi Gabriella  Gambino  alioutuma kwa washiriki wa  Mkutano  wa XXIV wa kichungaji wa familia huko Guatemala, Amerika ya Kusini uliofanyika mapema mwezi huu. Bi gambino amesema:“Iwapo tunataka kulinda na kutetea maisha tunapaswa kulinda wazee na kufanya kazi pamoja ili kuunda mzunguko wa mtandao wa uwepo na mshikamano wa kibinadamu na kikristo. Kuwatunza wazee ni kama kuwa na utunzaji wa Kristo aliye Maskini” amethibitisha Bi  Gambino katika ujumbe wake.

Wazee ni lengo la kupewa kipaumbele ndani ya matendo ya kichungaji ya kifamilia

Mkutano huo ambao umeudhuliwa na baadhi ya mamia ya watu kutoka katika majimbo yote ya nchi, umeongozwa na mada ya "ulinzi wa maisha"  kwa namna ya pekee kwa ajili ya wazee na ambayo ndiyo lengo kuu la kuzingatia na kutoa kipaumbele kama kiungo cha kutolea umakini wa rika hili la tatu ndani ya matendo ya kichungaji ya kifamilia. Kwa kuzingatia hilo, ujumbe wa Bi Gambino unaendelea kusema: “ uchaguzi wa kuwa na umakini ndani ya nafasi kubwa ya mantiki ya kichungaji ya kifamilia, ndiyo tunda la utambuzi ni kwa jinsi gani wazee ni tunu kwa ajili ya familia na ni kwa jinsi gani familia ni tunu kwa ajili ya wazee.”

Ulinzi wa maisha ya wazee pia ni jukumu la Kanisa

Ulinzi wa maisha ya wazee ni jukumu pia la Kanisa kwani “mahali ambapo kuna familia halisi ambayo haiwezi kujitunza yenyewe, jumuiya zetu zinaalikwa kuonesha uso wao wa huruma na kugeuka kuwa familia kwa yule ambaye amebaki na upweke katika wakati wake wa uzee”, amesisitiza. Hata hivyo Ujumbe wake umekuwa pia ni fursa ya kuwaalika baadhi ya wawakilishi wa Baraza la Maaskofu nchini Guatemala katika kushiriki Mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa kichungaji kwa ajili ya wazee  uliondaliwa na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha Mwezi huu Novemba. Kwa maelezo zaidi unaweza kusoma kupita tovuti hii: http://www.laityfamilylife.va/content/laityfamilylife/en/news/2019/gli-anziani-preziosi-per-la-famiglia--la-famiglia-preziosa-per-g.html

 

 

25 November 2019, 10:24