Tafuta

Nyumba mpya ya kwa ajili ya watu wasio kuwa na makazi imezinduliwa mjini Vatican ambapo Baba Mtakatifu jioni Ijumaa 15 Novemba 2019 amepata chai ya jioni na wageni hao Nyumba mpya ya kwa ajili ya watu wasio kuwa na makazi imezinduliwa mjini Vatican ambapo Baba Mtakatifu jioni Ijumaa 15 Novemba 2019 amepata chai ya jioni na wageni hao  

Jengo jipya la wasio kuwa na makazi mjini Vatican!

Kardinali Konrad Krajewski anatoa taarifa kuwa katika fursa ya Maadhimishi ya Siku ya III ya Maskini Duniani,Baba Mtakatifu Francisko jioni ya tarehe 15 Novemba 2019 ametembelea na kuzindua Kituo kipya cha mapokezi ya usiku na mchana kwa ajili ya watu wasio kuwa na makazi.Jengo hilo ni mali ya Vatican,na lipo meta chache kutoka nguzo za Uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican.

Kardinali Krajewski Msimamizi wa kitume wa sadaka ya Papa anatoa taarifa kuwa  katika fursa ya Maadhimishi ya Siku ya III ya Maskini Duniani, Baba Mtakatifu Francisko jioni ya tarehe 15 Novemba 2019 ametembelea na kuzindua Kituo kipya cha mapokezi ya usiku na mchana kwa ajili ya watu wasio kuwa na makazi. Jengo hilo liko meta chache kutoka katika nguzo za uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican katika neo la Mashariki na ni mali ya Vatican.

Jengo hilo lilikuwa linatumiwa na shirika moja  la watawa ambalo wameliacha miezi michache iliyopita na kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko amependelea kuliweka katika mantendo ya upendo kwa watu wenye kuhitaji na wenye matatizo. Jengo hili la Vatican limewakabidhiwa mfuko wa Kitume na ambapo litaendeshwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio kwa ushirikiano wa pamoja. Kituo cha mapokezi ya mchana na usiku katika Jengo liitwalo Palazzo Migliori, linachukua jina la familia iliyotoa zawadi kwa Vatican kunako mwaka 1930. Ni jengo lililojengwa kunako mwanzoni mwa mwaka 1800. Ndani yake lina unakishi  mzuri na linalowezesha hata wazee na watu wenye ulemavu kuweza kukaa. Katika Gorofa ya kwanza kuna Kikanisa kidogo kwa ajili ya sala binafsi na jumuiya ya watu wa kujitolea na wageni ambao wameo na wataweza kufika.

Vyumba vya kulala wakati wa usiku vitakuwa katika orofa ya tatu na ya nne na wataweza kuwapokea wanaume hata wanawake kufikia idadi ya watu 50 hivi ,lakini idadi inaweza kuongezeka kufuatana na ongezeko la baridi. Wageni watakao karibishwa usiku wataweza pia kupata chai ya asubuhi na chakula cha cha jioni kitakacho andaliwa. Hata hivyo katika Jiko la katikati na ambalo limetengenezwa kwa ustadi litasaidia kikundi cha watu wa kujitolea na mashemasi wa kudumu wa Roma kuweza kuandaa vizuri  zaidi sahani 250 za chakula cha moto na ambao kwa miaka kadhaa kila jioni wamekuwa wakisambaza kwa masikini na katika kesi hiyo ni katika vituo vya treni kama vile Termini, Tiburtina Ostiense.

katika orofa ya kwanza na ya  pili, kuna hata ofisi mbalimbali za kufanyia mazungumzo na kuwasikiliza wahitaji vile vile hata computa, za kuweza kujisomea na kukaa kwa pamoja katika shughuli za mafunzo na utamaduni ambapo watu wa kujitolea wataweza kuwasaidia watu hao. Shughuli zote za kazi ya kuikarabati jengo hilo zimefuatiliwa na kikundi cha watu wasio kuwa na makazi na kampuni moja maalum, ambapo ni ofisi ya Sadaka ya kitume ambayp imefadhili ukarabati huo na kwa njia ya michango inayotokana na baraka za kitume na kwa njia ya ukarimu wa sadaka ya watu binafsi. Pamoja na hayo Mfuko wa sadaka ya Kitume wa  Vatican pamoja na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio wanajitahidi uendelea kusaidia mpango huo kifedha katika shughuli zote za kusaidia wahitaji hao.

15 November 2019, 16:52