Tafuta

Vatican News
Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican umegeuka kuwa hotel kubwa ya kuwapokea wote katika maadhimisho ya Siku ya Maskini duniani 17 Novemba 2019 Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican umegeuka kuwa hotel kubwa ya kuwapokea wote katika maadhimisho ya Siku ya Maskini duniani 17 Novemba 2019  (Vatican Media)

Chakula cha mchana cha Baba Mtakatifu Francisko na maskini!

Katika hali ya mapokezi ya ukarimu wa kifamilia katikati ya uwepo wa Baba Mtakatifu Francisko na masikini,wameweza kupata mlo wa mchana mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana,katika fursa ya Siku ya Maskini duniani na ambapo ukumbi wa Paulo VI umegeuka kuwa hotel kubwa ya kuwapokea wote.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kwa mujibu wa Msemaji Mkuu wa Vatican amesema kuwa kabla ya kuanza chakula  cha mchana katika fursa ya Siku ya III ya Maskini Duniani, Baba Mtakatifu Francisko amezungumza maneno machache ya kuweza kawakaribisha wote na kusema kuwa: "Asante kuja kwenu. Ni mategemeo yangu kuwa Bwana atatubariki wote  leo hii  na pia Mungu kubariki mkutano  wetu na marafiki katika mlo huu na familia zenu. Bwana atubariki wote. Asante na mlo mwema”.

Watu karibia 150 wameweza kuhudumia na watu wa kujitolea 50

Hata hivyo katika simu ya Studio za Vatican News, Bwana Carlo Santoro wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ameweza kuelezea kwa kifupi hali halisi ilivyokuwa inaendelea katika ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican. Katika maelezo yake amesema kwamba walikuwapo watu 50 wa kujitolea kutoka katika parokia za Roma, ambao wameweza kuhudumia meza 150 zilizoandaliwa kwa watu karibia 1,500 wenye shida na ambao wanatoka katika mparokia ya wilaya ya Roma na majimbo katoliki ya Mkoa wa Lazio. Vile vile hata wengine wameweza kufika kutoka majimbo katoliki ya Italia kwa ujumla na ambao wamesindikizwa na watu wa vyama vya kujitolea. Chakula kilichotayarishwa kilikuwa rahisi cha aina ya pasta iitwayo “lasagnetta”, kuku na supu ya uyoga, viazi, keki, matunda na kahawa.

Lazima ndugu wote wahitaji kuhisi urafiki na ukaribu

Kwa hakika marafiki hawa wamehisi vizuri kama wako nyumbani, kwa maana ya kuhisi kulindwa, kupendwa na ndiyo wajibu wao kama Jumuiya ya Mtakatifu Egidio yaani "kuhisi kuwa nyumbani na siyo kubaguliwa", amesisitiza Bwana Santoro. Kwa maana hiyo amekumbusha hata maneno ambayo Baba Mtakatifu Francisko amesema kuhusu ndugu zetu hawa kuwa  wanahitaji “urafiki na ukaribu”. Nia kuu ya Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ni kuendeleza ule  wito wa Baba Mtakatifu ambao mara nyingi anakazia juu ya “ kupambana na utamaduni wa ubaguzi”. "Ni furaha kubwa kama Jumuiya kuona kwamba kila mwaka hali halisi kama hiyo inawafikia na kuwakumbatia watu wengi katika sehemu mbalimbali za dunia",amebainisha Bwana Santoro.

Mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko yamewagusa

Hata hivyo Bwana Santoro akielezea juu ya hisia ya ndugu hawa walioshiriki Misa Takatifu na baadaye mlo wa mchana, anafikiri kwamba kila mmoja na hata wao wenyewe wameguswa sana na maneno ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa mahubiri yake  na kila mmoja wa maskini anatambua vema ni kwa jinsi gani Baba Mtakatifu anawapenda sana, yeye ni rafiki mkubwa pia wanahisi kulindwa na kupokelewa na yeye. Uwepo wao katika ukumbi ule umewafanya wahisi kuwa nyumbani hasa kwa kuzingatia kwamba ukumbi wa Paulo VI, uligeuka kuwa hotel kubwa na katikati yake alikuwapo Baba Mtakatifu Francisko, lakini hakuwa  katikati peke yake, bali alikuwa pamoja na maskini wote! kwa maelezo zaidi ya mahubiri: https://www.vaticannews.va/sw/pope/news/2019-11/siku-ya-masikini-duniani-2019-tunu-ya-kanisa.html

JUMUIYA MT EGIDIO
17 November 2019, 15:03