Tafuta

Vatican News
Tarehe 16 Novemba Baba Mtakatifu mekutana mjini Vatican na Rais wa jamhuri ya Cape Verde Bwana Jorge Carlos de Almeida Fonseca Tarehe 16 Novemba Baba Mtakatifu mekutana mjini Vatican na Rais wa jamhuri ya Cape Verde Bwana Jorge Carlos de Almeida Fonseca   (Vatican Media)

Baba Mtakatifu amekutana na Rais wa Jamhuri ya Cape Verde

Tarehe 16 Novemba 2019,Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Rais wa Jamhuri ya Cape Verde Bwana Jorge Carlos Almeida Fonseca mjini Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Rais wa Jamhuri ya Cape Verde Bwana Jorge Carlos Almeida Fonseca, tarehe 16 Novemba 2019 mjini Vatican na ambaye baadaye amekutana na Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, akisindikizwa na Katibu Mkuu msaidizi wa mahusiano na nchi za Nje, Monsinyo Mirosław Stanisław Wachowski. Katika mazungumzo yao wameonesha uhusiano wao mzuri uliopo  na kuona jitihada zao za Mkataba kati ya Vatican na Jamhuri ya Cape Verde za mwaka 2014.

Kwa mujibu wa msemaji Mkuu wa Vyombo vya habari Vatican anasema, wakati wa mkutano wao, sehemu zote mbili wameridhishwa na hatua chanya za hivi karibuni zilizo chukuliwa za kuongezea katika mkataba wao wa makubaliano, huku wakiwa na matarajio ya kukamilishwa kwake kwa wakati ujao. Vile vile umuhimu wa elimu ya kimaadili na kidini katika shule ya Jamhuri ya nchi hiyo wameweza kuigusia na kwa ajili ya kuhamasisha thamani za familia na jamii. Vile vile wamegusia hata mchakato wa kumtangaza mwenye heri mtumwa Manuel, mwenye asili ya  nchi ya Cape Verde. Wakati wa mazungumzo yao pia masuala mengine yenye tabia ya kimataifa na kikanda na miongoni mwake ikiwa ni  matukio ya uhamiaji na ulinzi wa amani katika Afrika ya Magharibi.

16 November 2019, 14:28