Papa Francisko amemwongezea utume Askofu mkuu Novatus Rugambwa kwa kumteua kuwa Balozi wa Visiwa vya Marshall, Kiribati, Nauru na Tonga. Ataendelea kuwa pia Balozi New Zealand. Papa Francisko amemwongezea utume Askofu mkuu Novatus Rugambwa kwa kumteua kuwa Balozi wa Visiwa vya Marshall, Kiribati, Nauru na Tonga. Ataendelea kuwa pia Balozi New Zealand. 

Papa Francisko amwongezea Majukumu Askofu mkuu NOVATUS Rugambwa

Askofu mkuu Novatus Rugambwa alizaliwa tarehe 8 Oktoba 1957, nchini Tanzania, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 6 Julai 1986. Akajiunga na utume wa kidiplomasia mjini Vatican hapo tarehe 1 Julai 1991. Na Mwaka 2007 Papa Mstaafu akamteuwa kuwa Katibu mkuu msaidizi. Mwaka 2010 akateuliwa kuwa Askofu mkuu na Balozi na kuwekwa wakfu tarehe 18 Machi 2010.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu mkuu Novatus Rugambwa kuwa Balozi mpya wa Vatican kwenye Visiwa vya Marshall, Kiribati, Nauru na Tonga. Ataendelea pia kuwa ni Balozi wa Vatican nchini New Zealand, Fiji, Palau na Mwakilishi wa Kitume kwenye Bahari ya Pacific. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Novatus Rugambwa alizaliwa tarehe 8 Oktoba 1957, Katika Jimbo Katoliki la Bukoba nchini Tanzania. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre mikononi mwa Askofu Nestorius Timanywa kunako tarehe 6 Julai 1986. Akajiunga na utume wa kidiplomasia mjini Vatican hapo tarehe 1 Julai 1991. Baada ya kufanya kazi mbali mbali katika Balozi za Vatican, kunako tarehe 28 Juni 2007 Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto wa XVI akamteuwa kuwa Katibu mkuu msaidizi wa Baraza la Kipapa la shughuli za kichungaji kwa ajili ya wakimbizi na watu wasiokuwa na makazi maalum.

Ilipofika tarehe 6 Februari, 2010, Baba Mtakatifu Mstaafu  Benedikto XVI, akamteuwa kuwa  Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini Angola, Sao Tome na Principe na kuwekwa wakfu kuwa Askofu mkuu na Kardinali Tarcisio Bertone, aliyekuwa Katibu mkuu wa Vatican kwa wakati ule hapo tarehe 18 Machi 2010. Na tarehe 5 Machi 2015 akateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Honduras. Na kunako  tarehe 29 Machi  2019, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa  Balozi wa Vatican huko  New Zealand na mwakilishi wa kitume kwenye visiwa vya Bahari ya Pacific.

Askofu Mkuu Novatus Rugambwa
30 November 2019, 15:16