Askofu mkuuNicolas Henry Marie Denis Thevenin ameteuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Misri na Mwakilishi wa Kitume kwenye Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu. Askofu mkuuNicolas Henry Marie Denis Thevenin ameteuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Misri na Mwakilishi wa Kitume kwenye Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu. 

Askofu mkuu Nicolas Thevenin sasa ni Balozi nchini Misri na UAE

Askofu mkuu Thevenin alizaliwa mwaka 1958 huko, nchini Ufarans. Akapewa Daraja Takatifu mwaka 1989. Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI, tarehe 15 Desemba 2012 akamteuwa kuwa ni Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini Guatemala. Akawekwa wakfu na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI hapo tarehe 6 Januari 2013 kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Nicolas Henry Marie Denis Thevenin kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Misri na Mwakilishi wa Kitume kwenye Umoja wa Falme za Kiarabu. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Nicolas Henry Marie Denis Thevenin alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Guatemala. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Thevenin alizaliwa tarehe 5 Juni 1958 huko Saint-Disier, nchini Ufaransa. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 4 Julai 1989.

Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI, tarehe 15 Desemba 2012 akamteuwa kuwa ni Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini Guatemala. Akawekwa wakfu na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI hapo tarehe 6 Januari 2013 kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.  Askofu mkuu Nicolas Henry Marie Denis Thevenin alianza utume wake wa Kidiplomasia mjini Vatican tarehe 1 Julai 1994. Na tangu wakati huo, ametekeleza utume huu nchini DRC, Ubelgiji, Lebanon, Cuba, Bulgaria na hatimaye, Vatican kwenye Sekretarieti kuu ya Vatican na Guatemala.

04 November 2019, 14:03