Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Dominic Kimengich kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Eldoret, nchini Kenya. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Dominic Kimengich kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Eldoret, nchini Kenya. 

Askofu Dominic Kimengech, sasa anaongoza Jimbo la Eldoret, Kenya

Askofu Dominic Kimengich ameteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Eldoret. Kabla ya uteuzi huu, Askofu Kimengich alikuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Lodwar. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Maurice Crowley wa Jimbo Katoliki la Kitale, kuwa ni Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki la Lodwar. Jimbo la Eldoret limekuwa wazi kufuatia kifo cha Askofu C. Korir.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu Dominic Kimengich kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Eldoret, nchini Kenya. Kabla ya uteuzi huu, Askofu Kimengich alikuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Lodwar. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Maurice Crowley wa Jimbo Katoliki la Kitale, kuwa ni Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki la Lodwar. Jimbo Katoliki la Eldoret limekuwa wazi kufuatia kifo cha Askofu Cornelius Korir kilichotokea tarehe 30 Oktoba 2017.  Ilikuwa ni tarehe 20 Machi 2010, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI alipomteuwa kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Lodawar na kuwekwa wakfu kama Askofu tarehe 22 Mei 2010 na Kardinali John Njue, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Nairobi. Tarehe 5 Machi 2011, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Lodwar na tarehe 16 Novemba 2019, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Eldoret.

Kwa ufupi, itakumbukwa kwamba, Askofu Dominic Kimengich alizaliwa tarehe 23 April, 1961 huko Kituro, Wilaya ya Baringo, Jimbo Katoliki la Nakuru. Alipata majiundo yake ya Falsafa kwenye Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino na baadaye masomo ya kitaalimungu ameyapatia huko Seminari kuu ya Mtakatifu Thomas wa Akwino, iliyoko Jimbo kuu la Nairobi, Kenya. Aliendelea na masomo na hatimaye kujipatia shahada ya uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Santa Croce, kilichoko mjini Roma. Tarehe 14 Septemba, 1986, Siku kuu ya Kutukuka kwa Fumbo la Msalaba, Askofu Kimengich alipewa daraja takatifu ya Upadre na kupokelewa Jimbo Katoliki la Nakuru. Baada ya upadrisho alifanya shughuli mbali mbali za kichungaji Parokiani kama Paroko Msaidizi, Gambera wa seminari ndogo, Makamu wa Askofu na Mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu. Kuanzia Mwaka 2007-2008 aliteuliwa kuwa Gambera wa Seminari kuu ya Mtakatifu Mathias Mulumba, iliyoko Tindinyo. Amewahi kushika nyadhifa kama: Hakimu wa Mahakama ya Jimbo la Nakuru, mjumbe wa Kamati ya Liturujia, Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya na mjumbe wa Tume ya Mafundisho ya Imani, Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya.

Askofu Eldoret

 

18 November 2019, 09:07