Tafuta

Vatican News
5 Oktoba 2019:Ziara ya Makardinali wapya kumtembelea Papa Benedikto XVI 5 Oktoba 2019:Ziara ya Makardinali wapya kumtembelea Papa Benedikto XVI  (Vatican Media)

Ratzinger kwa makardinali wapya amewasihi wakumbuke thamani ya uaminifu kwa Papa!

Mara baada ya maadhimisho ya Misa ya kusimikwa kwa makardinali wapya,Baba Mtakatifu Francisko na makardinali hao wapya wamekwenda kumwona Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI katika Monasteri ya “Mater Ecclesiae”.

Tarehe 5 Oktoba 2019 majira ya jioni hivi, mara baada ya kuhitimishwa madhimisho ya kusimikwa kwa makardinali wapya, Baba Mtakatifu Francisko pamoja na  Makardinali wapya wamekwenda kwa Bus ndogo hadi kwenye Monasteri ya “Mater Ecclesiae” mjini Vatican ili kukutana na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI. Hayo ni kwa mujibu wa msemaji Mkuu wa Vyombo vya habari Vatican Dk. Matteo Bruni.

Baada ya salam fupi pia kuwakumbusha makardinali wapya juu ya thamani ya uaminifu kwa Papa, Baba Mtakatifu Mstafu Benedikto XVI pamoja na Baba Mtakatifu Francisko wamewabariki makardinali kwa kwa baraka yao. Na hatimaye Makardinali wapya  wamerudi katika ukumbi wa Papa Paulo VI na katika Nyumba ya Kitume kwa ziara ya faragha na wakati huo huo Baba Mtakatifu Francisko akarudi nyumbani kwake katika Nyumba ya Mtakatifu Marta.

05 October 2019, 18:59