Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amepata nafasi ya kukutana na kusalimiana na wajumbe maalum waliofika mjini Vatican katika Ibada ya kuwatangaza watakatifu wapya 13 Oktoba 2019. Baba Mtakatifu Francisko amepata nafasi ya kukutana na kusalimiana na wajumbe maalum waliofika mjini Vatican katika Ibada ya kuwatangaza watakatifu wapya 13 Oktoba 2019. 

Watakatifu Wapya 2019: Wajumbe Maalum waliohudhuria Misa

Ibada hii imehudhuriwa na wajumbe maalum kutoka: Italia, Uingereza, Brazil, Taiwan, Ireland na Uswiss. Ujumbe wa Italia umeongozwa na Rais Sergio Mattarella wa Italia, Ujumbe wa watu 15 kutoka Uingereza ulikuwa chini ya Mtoto wa Mfalme Carlo, Ujumbe wa watu 6 kutoka Taiwan umeongozwa na Bwana Chen Chien-Jen, Makamu wa Rais wa Taiwan. Brazil ilikuwa na wajumbe 23.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumapili tarehe 13 Oktoba 2019 amewatangza Wenyeheri wafuatao kuwa ni watakatifu katika Ibada ya Misa Takatifu iliyoadhimishwa kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu wa Mungu kutoka sehemu mbali mbali za dunia. Watakatifu wapya ni: Kardinali John Newman, muasisi wa Kituo cha Michezo cha Mtakatifu Filippo Neri kilichoko nchini Uingereza. Sr. Giuseppina Vannini, Muasisi wa Shirika la Mabinti wa Mtakatifu Camillus; Maria Theresa Chiramel Mankidiyan, Muasisi wa Shirika la Watawa wa Familia Takatifu; Sr. Dulce Lopes Pontes wa Shirika la Watawa Wamisionari wa Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili na Mama wa Mungu pamoja na Margarita Bays, Bikira na mtawa wa Utawa wa tatu wa Mtakatifu Francisko wa Assisi.

Ibada hii imehudhuriwa na wajumbe maalum kutoka: Italia, Uingereza, Brazil, Taiwan, Ireland na Uswiss. Ujumbe wa watu 16 kutoka Italia umeongozwa na Rais Sergio Mattarella wa Italia, Ujumbe wa watu 15 kutoka Uingereza ulikuwa chini ya Mtoto wa Mfalme Carlo, Ujumbe wa watu 6 kutoka Taiwan umeongozwa na Bwana Chen Chien-Jen, Makamu wa Rais wa Taiwan. Ujumbe wa Brazil uliokuwa na watu 23 ulikuwa chini ya uongozi wa Bwana Martins Mourao, Makamu wa Rais. Kulikuwa na wajumbe 3 kutoka Ireland walioongozwa na Bwana Joe McHugh, Waziri wa elimu nchini Ireland. Na mwishoni katika orodha hii, walikuwa ni wajumbe 8 kutoka Uswiss chini ya uongozi wa Mama Karin Keller-Sutter, Mshauri katika Serikali ya Wananchi wa Uswiss.  Kama kawaida ya matukio kama haya, Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya maadhimisho ya Ibada ya Misa Takatifu amepata nafasi ya kusalimiana na wajumbe hawa huku akiwashukuru kuwa uwepo wao pamoja na kuwatakia heri na baraka kwa ajili ya nchi wanamotoka!

Wageni Maalum

 

 

13 October 2019, 14:57