Katika fursa ya Sinodi ya Maaskofu kuhusu Amazonia inayoendelea,imefanyika mjini Vatican Njia ya Msalaba kwa ajili ya kuwakumbuka wafiadini wa Amazonia Katika fursa ya Sinodi ya Maaskofu kuhusu Amazonia inayoendelea,imefanyika mjini Vatican Njia ya Msalaba kwa ajili ya kuwakumbuka wafiadini wa Amazonia 

Njia ya msalaba kwa ajili ya kukumbuka wafiadini na watu wa Amazonia!

Kuanzia Castel Sat’Angelo na kupitia njia ya Conciliazione hadi katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,waamini wa mataifa yote na mababa wa Sinodi tarehe 19 Oktoba mchana wamefanya Njia ya Msalaba kwa ajili kuombea wafiadini na hata ya haki ya msitu mkubwa wa dunia wa Amazonia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Njia ya Msalaba imefanyika kuanzia Castel Sant’Angelo kupitia njia ya Conciliazione hadi kwenye uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican tarehe 19 Oktoba 2019 kwa ajili ya kukumbuka leo hii wafiadini na haki zinazo kiukwa za Msitu wa Amazonia na ambayo ndiyo mada kuu inayoendelea katika Sinodi ya Maaskofu mjini Vatican. Hija ya njia ya msalaba imeandaliwa na Repam na kutoka nyumba ya pamoja ya Amazonia ambapo wameshiriki waamini wote kutoka pande za  duniani wakiwa pamoja na baadhi ya mababa wa Amazonia wanaoshiriki Sinodi ya Maaskofu.

Kwa ajili ya wafiadini wa Amerika ya Kusini

Nyimbo za waamini zilikuwa zikitumbuizwa huku zikikumbusha vurugu na kusongwa kwa watu wa asilia wa Amazonia. Walikuwapo watu wa asili, wakiwa wamevaa mavazi yao ya asilia hata zana za kiutamaduni na kutembea kupitia njia ya Conciliazione wakisali, na kusimama katika Kanisa la Mtakatifu Maria Traspontina katikati ya njia ya Conciliazione ambapo kilikuwa ni kituo cha njia ya msalaba cha sala. Katika kila kituo cha Njia ya Msalaba waliweza kuwakumbuka kila mfiadini wa Amerika ya Kusini na kila moja ya haki zilizo kiukwa na zinazo endelea kukiukwa  huko Amazonia. Kwa hakika ni watu wengi wanaoteseka katika mazingira na kama ilivyo hata suala la ukataji miti hovyo na unyonyaji wa mafuta.

Msalaba kwa ajili ya msitu

Picha ya Amazonia na watu wake waliweza kuziwakilisha na kuziweka karibu na msalaba na wakati huo huo  waamini wengine walikuwa wakiandika juu ya kitaambaa kikubwa cheupe mawazo yao kwa ajili ya kuunga mkono juu ya wokovu wa msitu mkubwa wa Amerika Kusini. Wakati wa hitimisho la Njia ya Msalaba wamefunua hata baadhi ya michoro ya Adolfo Pérez Esquivel, mwanaharakati wa amani kutoka Argentina na Mtuzwa Nobel ya amani mwaka 1980.

Kardinali Barretto: Amazonia inarudi kuwa kiini

Kati ya mababa wa Sinodi alikuwapo hata Kardinali  Pedro Ricardo Barreto Jimeno, Askofu Mkuu wa Huancayo na makamu Rais wa Mtandao wa Kanisa wa Amazonia (REPAM). Wakati wa kutoa neno amesema: "watu wa asilia ndiyo wako mstari wa mbele katika ndoto hiyo na ambayo inakaribia kuwa hali halisi, kuanzia pembezoni mwa maisha hadi kufikia eneo la kijiografia ambalo ni Amazonia, pia ni  kiini kama ilivyo cha ukristo ambao ni Roma. Njia ya Msalaba ina maana kuwa Kristo yupo nasi na anatusindikiza, anateseka na ndugu na kwa maana hiyo tumshukuru Mungu kwa kuwa tupo tunaishi ufufuko wake, furaha  ya Injili."

20 October 2019, 09:30