Vatican News
Katika uwasilishaji kuhusu Sinodi kwa waandishi wa habari alikuwapo Askofu Mkuu Fissichella, Mauricio Lopez Katibu mtendaji wa Repam na Sr. Daniela Adriana Katibu  Mkuu wa Clar nchini (Colombia) Katika uwasilishaji kuhusu Sinodi kwa waandishi wa habari alikuwapo Askofu Mkuu Fissichella, Mauricio Lopez Katibu mtendaji wa Repam na Sr. Daniela Adriana Katibu Mkuu wa Clar nchini (Colombia) 

Sinodi:kati ya mapendekezo mengi kuna ibada ya Amazonia!

Tarehe 18 Oktoba 2018 wamesilisha kwa waandishi wa habari kuhusu taarifa za mikutano ya makundi madogo madogo ya Sinodi Maalum ya Maaskofu mjini Vatican.Waliozungumza ni Askofu Mário Antônio da Silva,wa Roraima (Brazil),Askofu Mkuu Rino Fisichella,Rais wa Baraza la Kipapa la kuhamaisha uinjilishaji mpya,Mauricio Lopez,Katibu mtendaji wa Repam na Sr.Daniela Adriana Cannavina,katibu mkuu wa Clar (Colombia)

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican

Wakati wa ufunguzi wa kuwakilisha kwa waandishi wa habari kuhusu ripoti ya duru 12 ya  mikutano katika makundi madogo madogo, wanasema ripoti  bado hayajakamilika lakini ni hatua mojawapo amabayo imezaliwa kutokana na kusikiliza na kuelekeza kwenye mang’amuzi. Katika baadhi ya makundi, majadiliana na makabiliano yalikuwa yamefunguliwa wazi. Nafasi za mawazo ya  mababa za wa Sinodi siyo mara nyingi zinakwenda sambamba lakini kila mtu anatoa mchango wake binafsi. Kwa mujibu wa utangulizi huo Padre  Giacomo Costa, katibu wa Tume ya Habari, alifungua mkutano kwa waandishi wa habari kwa uwasilishaji wa ripoti za Duru ndogo 12  za mikutano kuhusu sinodi inayoendelea na ambayo itafungwa tarehe 27 Oktoba 2019.

Upyaishwaji na kukuza maana ya maisha ya kitawa

Kuhusu Sinodi ya Kanda ya Amazonia pia umetolewa ushauri na Sr. Daniela Adriana Cannavina, ambaye ni Katibu Mkuu wa Clar (Colombia) ambaye amesisitiza kwamba wito ni ule wa kufikiria Amazonia na kufungua hatua mpya kwa ajili ya Kanisa. Ni lazima kutoa uwezekano wa kufanya mazoezi  ya dhati  ya kushinda hofu. Vile vile amekumbuka kuwa wakati wa kazi ya Sinodi kumekuwapo na nafasi ya kutoa mchango kwa upande wa  wanawake. Akigusia kuhusu maisha ya kitawa ameelekeza njia mwafaka ya kuendelea kuhamasisha maisha yanayo jikita juu ya Injili. Ni lazima kuvumilia dhidi ya sintofahamu kwa sababu, maisha ya kitawa ni picha ya ukarimu wa maisha. Sr. Daniela aidha ameelekeza funguo  nne msingi wa kuweza kufuata: wa kwanza ni utumadunisho,  pili kusafiri kwa maana ni uhakikisho wa Kanisa linalotoka nje. Na funguo mbili msingi ni ufunguzi wa njia mpya ili ziimarishe uwepo wa wamisionari ambao wanede na karama na kuhamasisha majadiliano kati ya wachungaji, na walei katika mazingira ya kuwajibika.

Kuzuia dhambi za kiekolojia

Hata hivyo kuunda uchunguzi wa mazingira huko Amazonia, ili kuzuia dhambi za kiekolojia", ni moja ya mapendekezo yaliyoibuka kutoka Sinodi, inayoendelea mjini Vatican hadi Oktoba 27 Oktoba na ambayo yamo kwenye ripoti  za Duru ndogo 12 zilizowasilishwa tarehe 18 Oktoba 2019 katika ofisi ya waandishi wa habari ya Vatican. Naye Askofu Rino Fischella, Rais wa Baraza la Kipapa la uhamasishaji wa uinjilishaji mpya akijibu swali la waandishi wa habari linalotokana na mjadala kuhusu dhambi za kiutamaduni, amesema, dhambi za kiekolojia kwa uharibifu wa kazi ya uumbaji na mazingira, ina sura moja, ambayo baadaye inagawanyika katika sura tofauti. Hii inazaliwa ndani yenyewe, katika ubinafsi kwa yule ambaye anaishi, anayethubutu kufa kwa ajili ya kukosa hewa na bila kutambua kuwa uasili, maisha na uhusiano vinaalika kuwa na mtazamo mpana, uliopo na ujao.

Tabia ya mwanadamu ya kujifunga binafsi

Zaidi ya ugawanyaji au kuzidishwa kwa dhambi, kuna dhambi  msingi ambayo inakaa katika tabia ya mwanadamu na ambayo humfunga mbele za Mungu,na kazi ya uumbaji  yenye udhihirisho wa Mungu. Ni mtazamo wa ulimwengu kwa kila mtu, ambaye hujifunga mwenyewe na hataki kukubali maono yenye nguvu na mapana ya kuishi. Vile vile Ekolojia fungamani ina lengo kubwa na ambayo utupelekea katika uongofu wa kiekolojia kwa mujibu wa Askofu Mário Antônio da Silva, wa jimbo la Roraima, nchini  Brazil, na kuongeza kusema kuwa “Kila kitu ambacho kinatupeleka na kutuongoza  katika  matumizi ya lazima, ya uwajibikaji na busara wa mali za  uumbaji siyo dhambi , bali ni  wema, wakati  huo huo kila kitu ambacho kinatuongoza kwenye faida kubwa, inayozidi, siyo tu kunuka lakini pia ina kinasaba chake cha   dhambi, uovu, katika ukosefu wa haki. Hili siyo suala la kuunda orodha ya dhambi, lakini ni ile ya  kutekeleza uongofu wa kiekolojia ambao Baba Mtakatifu alipendekeza kwetu sisi katika Wosia wake waLaudato sì na ambao lazima uongoze maisha yetu yote”.

 

19 October 2019, 11:35