Tafuta

Vatican News
Mababa wa Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia wameanza majadiliano katika vikundi, sehemu ya mchakato wa maandalizi ya muswada wa hati ya Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia. Mababa wa Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia wameanza majadiliano katika vikundi, sehemu ya mchakato wa maandalizi ya muswada wa hati ya Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia. 

Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia: Majadiliano ya Vikundi

Mababa wa Sinodi wanajadiliana yale mambo msingi ambayo yameibuliwa katika vikao vilivyopita. Hizi ni tema ambazo zitafanyiwa kazi tena kwa siku za usoni, ili kuweza hatimaye, kuwekwa kwenye muswada wa Hati ya Mababa wa Sinodi. Jumamosi tarehe 12 hadi Jumanne tarehe 15 Oktoba, Mababa wa Sinodi watarejea tena kwenye Ukumbi wa Sinodi kuendelea na majadiliano yao.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia kuanzia tarehe 6-27 Oktoba, 2019 yanaongozwa na Kauli mbiu: “Amazonia: njia mpya ya Kanisa na kwa ajili ekolojia fungamani”. Hii ni Sinodi inayoadhimishwa kwa kuzingatia mambo makuu manne: Shughuli za Kichungaji, Kitamaduni, Kisiasa na Kiekolojia; mambo ambayo ni sehemu muhimu ya ekolojia fungamani. Baadhi ya Tema zilizokwisha kujadiliwa hivi karibuni ni pamoja na: Utumwa mamboleo na changamoto ya toba na wongofu wa kiekolojia; Dhamana ya uinjilishaji na utamadunisho; Dhana ya Sinodi, ari na mwamko wa kimisionari; changamoto za maisha, wito na utume wa Kipadre; Njia mpya ya “Viri probati”.

Mababa wa Sinodi wamekazia umuhimu wa Kanisa kuhamasisha Ibada mbali mbali kama chemchemi ya malezi, majiundo na utakatifu wa maisha pamoja na majadiliano ya kidini, kiekumene na kitamaduni kwa ajili ya mafao ya wengi. Mababa wa Sinodi, baada ya kuwachagua waratibu na wazungumzaji wakuu wa vikundi wakati wa maadhimisho ya Sinodi, Alhamisi, tarehe 10 hadi Ijumaa tarehe 11 Oktoba 2019 wameanza majadiliano katika vikundi mbali mbali ili kuwawezesha Mababa wengi wa Sinodi kuweza kuchangia mawazo, mang’amuzi na vipaumbele vyao katika mchakato wa maisha na utume wa Kanisa Ukanda wa Amazonia.

Mababa wa Sinodi wanajadiliana yale mambo msingi ambayo yameibuliwa katika vikao vilivyopita. Hizi ni tema ambazo zitafanyiwa kazi tena kwa siku za usoni, ili kuweza hatimaye, kuwekwa kwenye muswada wa Hati ya Mababa wa Sinodi. Jumamosi tarehe 12 hadi Jumanne tarehe 15 Oktoba, Mababa wa Sinodi watarejea tena kwenye Ukumbi wa Sinodi kuendelea na majadiliano yao. Jumatano tarehe 16 hadi tarehe 17 Oktoba, Mababa wa Sinodi watakusanyika tena kwenye Vikundi, ili kuweza kukusanya mawazo makuu yaliyojitokeza, ili hatimaye, yaweze kuwasilishwa kwenye Sekretarieti kuu ya Sinodi. Ikumbukwe kwamba, kwa njia ya majadiliano ya vikundi, Mababa wa Sinodi wameanza pia kuandaa muswada wa Hati ya Mababa wa Sinodi, Muhtasari wa mambo msingi yaliyojitokeza wakati wa majadiliano.

Majadiliano ya Vikundi
11 October 2019, 14:36