Tafuta

Sinodi Maalumu kuhusu Amazonia inaendelea mjini Vatican ikiwa tayari imeingia wiki ya pili na inatarajiwa kufungwa tarehe 27 Oktoba 2019 Sinodi Maalumu kuhusu Amazonia inaendelea mjini Vatican ikiwa tayari imeingia wiki ya pili na inatarajiwa kufungwa tarehe 27 Oktoba 2019 

Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia:jitihada za Kanisa dhidi ya ukiukwaji wa haki za watu!

Katika kikao cha 9 cha Sinodi ya Maaskofu kuhusu Amazonia,tarehe 14 Oktoba asubuhi wameanza sehemu ya pili kati ya wiki tatu Maalum ya Kanda ya Amazonia.Mababa wa Sinodi waliokuwapo pamoja na Baba Mtakatifu wamesali hata kwa ajili ya nchi ya Ecuador.Na sehemu ya pili mchana kikao cha 10 wamefikiria kwa upya kuhusu huduma ya Kanisa katika nuru ya umbo la upamoja.

Vatican News

Sinodi ni Kairos, kipindi cha neema:Kanisa linajiweka kidete kwenye usikivu na kutembea karibu na watu wa asilia kwenye misitu. Maeneo ya pembezoni mwa kijiografia ya maisha ambayo wamepokea kama zawadi ya kutafakari kila siku kwa njia ya “Fiat” neno la kwanza lililotamkwa na Mungu. Uumbaji kwa hakika ni Biblia ya kijani ambayo  inayomwonesha Muumba na katika kuathimisha sakramenti, jitihada za kiekolojia ambayo inataka msingi wake wa kina. Ni katika kikao cha 9 cha Sinodi ya Maaskofu kuhusu Amazonia, tarehe 14 Oktoba asubuhi ambapo wameanza sehemu ya pili kati ya wiki tatu Maalum ya Kanda ya Amazonia. Mababa wa Sinodi waliokuwapo pamoja  na Baba Mtakatifu Francisko wamesali hata kwa ajili ya nchi ya Ecuador.Na sehemu ya pili mchana katika kikao cha 10 wamefikiria kwa upya kuhusu huduma ya Kanisa katika mwanga wa umbo la upamoja.

Mafunzo ya kudumu na wakatekumeni kwa ajili ya Kanisa linalotoka nje

Aidha mababa katika mkutano wao wamejikita kutazama hali halisi ya uendeshaji wa huduma za Kanisa kwamba mbele ya hali halisi ya upungufu wa jumuiya za kidini katika kanda, kama inavyojitokeza kwa mfano katika Serikali ya Para nchini Brazil, ni vema kuomba mashirika mbalimbali ya kitawa ili kutafuta namna ya kurudisha chachu na ari ya kimisionari. Na wakati huo huo, inahitaji kutoa mafunzo ya kuendelea na kutambea katika mchakato wa ukatekumene na siyo tu katika kujifunza kwenye vitabu vya mafunzo, lakini katika kufanya uzoefu kwenye nyanja ya moja kwa moja ya kukutana na utamaduni mahalia. Kuchukua majukumu ya sura ya Amazonia, ina maana ya kuelewa ishara na na mambo ya  watu hawa na kuishi kwa mtazamo wa majadiliano na utamadunisho, huku wakitiwa moyo wa kujikita kwa kina katika taalimungu ya kihindi, na ili liturujia iweze kujibu zaidi na daima  utamaduni mahalia. Kanisa linaitwa kukabiliana na  changamoto zilizojitokeza kwa upande mmoja na kutokana na kuenea  kwa madhehebu ya kidini mengine na kwa upande mwingine, tamaduni za ushirika zinazotoka katika nchi zilizoendelea kiviwanda.

Mchango kwa mantiki ya kimataifa

Aidha Kanisa linaalikwa kusikika sauti yake. Katika mkutano wao kadhalika kwa wanathibitisha kwamba  uwepo wa uwakilishi wa kipapa katika Serikali na mashrika ya Kimataifa unaweza kusaidia kuendeleza nafasi msingi na hatimaye kwa ajili  ya kuhamasisha maendeleo ya watu wa Amazonia, hasa katika haki zao  za  ardhi, maji na msitu. Na zaidi Kanisa la Amazonia linaalikwa kuhamasisha uchumi wa mzunguko, wa kuheshimu hekima na mazoezi ya watu mahalia.  Hata hivyo pendekezo kuunda  mwakilishi wa Kanisa Kimataifa kuhusiana  na ukiukwaji wa haki za binadamu katika watu wa Amazonia ni muhimu sana; kwa maana hiyo, nchi zenye viwanda zijielezee kuwa na mshikamano mkubwa kwa nchi na uchumi mdhaifu,  hata kwa sababu wao ndiyo wenye kuwa na uchafuzi  mkubwa wa hali ya hewa.

Mawasiliano yasaidie muunganisho

Amazonia ni dunia ya kabila nyingi, utamaduni mwingi na dini nyingi, mahali ambapo mbegu za Neno, zimekwisha na zipo zinatoa matunda mengi. Ni matumaini ya uundaji wa mfumo  wa mawasiliano ya kikanisa ya Amazonia ambayo yanajifafanua katika muunganiko wa ubinadamu mzima. Wazo ni lile la kusuka, si tu mtundao wa nyaya, lakini ni za utu wa kibinadamu. Matatizo mengi yanayoikumba kanda hiyo kwa hakika ni dhaurura inayohitaji mwafaka na njia za mawasiliano ya kiuchumi.  Inahitajika wakati  huo huo kuwasaidia watu wajitambue  na kugundua baadhi ya vyombo vya habari vinavyojificha nyuma ya  kila aina ya mitindo ya ujanja, upotoshaji na  tamasha.

kuthamanisha karama za waamini walei,mbali na ukleri

Katika kikao cha 10 cha Mababa wa Sinodi Maalum ya Maaskofu kuhusu Amazonia, mchana wakiwa pamoja na Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 14 Oktoba  wamendelea kufikiria kwa upya huduma ya Kanisa kwa mwanga wa maumbo ya upamoja. Hii ni moja ya changamoto ya Kanisa  huko Amazonia , ili Kanisa daima liweza kuwa la Neno. Aliyeonesha hayo ni baadhi ya hotuba zilizotangazwa katika ukumbi huo mchana na wageni wakaribishwa kusikiliza. Neno la Mungu ni uwepo hai  na huruma, inayofundisha na ya kinabii, inaunda na kuendeleza kufudisha, inayoalika kwa mantiki ya ekolojia fungamani na shara ya jitihada kijamii, kiuchumi , kiutamaduni na kisasa kwa ajili ya maendeleo ya ubinadamu mpya. Wanahitajika wahudumu wapya wa Neno, wakijumuishwa wanawake ili kutoa jibu jipya katika changamoto ya sasa na ni lazima kuwekeza kwa walei ambao wameandaliwa vema na wenye roho ya kimisionari, wanaotambua kutangaza Injili kwa kila kona la Amazonia; Mafunzo ya kutosha kwa walei  ni msingi hata kwa ajili ya kuzaliwa kwa miito mipya, wamesisitiza 

Uchungaji wa miito na uchungaji wa vijana

Aidha katika hotuba zao kwenye kikao, imejitokeza suala la umuhimu wa miito kichungaji. Hii inasisitiza kwamba haiwezekani kukosekana katika shughuli za uinjilishaji kama inavyotakiwa kuwasindikiza vijana kichungaji na wakati huo huo kuwa na mapendekezo ya kukutana binafsi na Kristo. Vijana wanatakiwa kumfuata Yesu  na hivyo lazima wasaidiwe katika mafunzo yanayotosha kwa njia ya ushuhuda wa maisha matakatifu na wanaojikita ndani humo. Mapadre wanapaswa wawe na uwezo wa kuelewa kwa kina mahitaji na dharura ya Amazonia. Katekesi yao isiwe kama ya darasani , lakini kuendeleza kwa roho ya kimisionari na moyo wa kichungaji.

Tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko

Wakati wa kuhitimisha kikao hiki cha 10 katika ukumbi, Baba Mtakatifu Francisko hatimaye  amerudi kutafakari baadhi ya mada zilizozitokeza katika kazi hiyo na kuonesha baadhi ya mambo yalioyo mgusa zaidi.

15 October 2019, 12:52