Imetolewa tamko rasmi ya maadhimisha ya sikukuu ya Bikira Maria wa Loreto kwa ngazi ya Kanisa la ulimwengu kila ifikapo tarehe 10 Desemba ya kila mwaka Imetolewa tamko rasmi ya maadhimisha ya sikukuu ya Bikira Maria wa Loreto kwa ngazi ya Kanisa la ulimwengu kila ifikapo tarehe 10 Desemba ya kila mwaka 

Tamko kuhusu Sikukuu ya Bikira Maria wa Loreto 10 Desemba!

Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa,tarehe 31 Oktoba imetoa tamko rasmi la Baba Mtakatifu Francisko kuridhia kuhusu Maadhimisho ya Bikira Maria wa Loreto ambapo itakuwa inaadhimishwa katika Kanisa la ulimwenguni kila tarehe 10 Desemba ya kila mwaka.Na 1 Novemba,misa ya ufunguzi wa jubilei ya Mama “Maria Regina et Janua Coeli.Itaanza rasmi tarehe 8 Desemba 2019 -10 Desemba 2010.

Alhamisi tarehe 31 Oktoba 2019, Baraza la Kipapa la nidhamu na Sakramenti za Kanisa limetangaza  Hati juu maandhimisho  ya sikukuu ya Bikira Maria wa Loreto iliyoaridhiwa na Baba Mtakatifu Francisko ili iweze kuingizwa katika kalenda kuu ya madhimisho ya liturujia zote. Hadi sasa kumbukumbu hiyo ilikuwa ikifanyika kwa ngazi ya Kanisa mahalia tu. Katika maelezo zaidi Kardinali Sarah Baraza la Kipapa la nidhamu na Sakramenti za Kanisa anaandika kuwa ibada  kwa ajili ya Nyumba Takatifu ya Loreto imeanza kwa kipindi kirefu  na asili ya Madhabahu hiyo hadi leo hii, imefikiwa na mahujaji kutoka pande za dunia kwa ajili ya kujiimarisha imani yao katika Neno lililofanyika mwili kwa ajili yetu sisi.

Katika madhabahu hiyoinakumbusha fumbo la Yesu aliyefanyika mwili na kutoa msukumo kwa wale ambao wanaitembelea na kufikiri utimilifu wa nyakati, wakati Mungu alipomtuma Mwanaye aliyezaliwa na  mwanamke, pia  kutafakari kwa kina juu ya maneno ya  Malaika aliyompasha habari, hata majibu ya Bikira Maria aliyojibu wito wa Mungu. Kufunikwa na kivuli cha Roho Mtakatifu na mnyenyekevu wa Bwana, kwa maana hiyo eneo hilo limegeuka kuwa nyumba ya Mungu, picha safi ya Kanisa Takatifu.

Madhabahu hiyo imekuwa pia moja kwa moja chini ya usimamizi wa Vatican na ambayo imepewa sifa na Mapapa  wote na duniani inajulikana sana na kuonesha kwa namna gani hata kwa kipindi chote cha nyakati haijatofautiana na mji wa Nazareth  katika nchi Takatifu zile fadhila za kiinjili za Familia Takatifu. Katika nyumba Takatifu, mbele  yake Picha ya Mama wa Mkombozi na wa Kanisa, Watakatifu na wenyeheri waliweza kujibu wito wake  huo huo; wagonjwa wanomba faraja katika mateso yao, watu wa Mungu walianza kusifu na kuomba Mtakatifu Maria kwa njia ya Litania ya Bikira Maria wa Loreto na nyimbo duniani kote. Kwa namna ya pekee ni lazima kukumbuka ni watu wangapi wanasafiri kwa ndege na wameweza kumtembelea, Mama kikao cha ibada.

Kardinali Robert Sarah, katika Hati hiyo anaandika  kuwa: katika mwanga wa hayo yote, Baraza la Kipapa la Ibada na Sakramenti za Kanisa limeamua kutekeleza uamuzi wa Baba Mtakatifu Francisko ambapo ametoa idhini kwamba badala ya maadhimisho ya Bikira Maria wa Loreto kuadhimishwa katika Kanisa mahalia sasa itadhimishwa kwa ngazi ya Kanisa la ulimwengu. Kadhali ili kuhakikisha kwamba, marekebisho haya yanaingizwa katika Kalenda ya Liturujia ya Kanisa, kila  tarehe 10 Desemba siku ambayo ni sikukuu ya Bikira Maria wa Loreto ambayo imekuwa ikiadhimishwa kila Mwaka.

Maadhimisho haya yatasaidia wote hasa familia, vijana, watawa  kuiga mfano wa fadhila timilifu  za mtume wa Injili, Bikira Maria ambaye katika kutunga mimba ya Mkuu wa Kanisa  na ambaye alitukaribisha hata sisi. Kumbukumbu hii kwa namna nyingine iwekwe mara moja katika kalenda na vitabu vyote vya kiliturujia za misa na liturujia za masifu; lakini pia tamko hili linayataka Mabaraza ya Maaskofu Katoliki sehemu mbali mbali za dunia kufanya hivyo hasa kutafsiri maelekezo ya maadhimisho ya Misa Takatifu na Sala ya Kanisa.

Ikimbukwe kuwa:Katika madhambahu ya Mama Maria wa Loreto, tarehe 1 Novemba 2019  saa 4.00  asubuhi majira ya Ulaya, itaadhimishwa misa Takatifu, ikiwa ni ufunguzi wa Jubilei  ya Mama “Maria Regina et Janua Coeli”, misa itakayoongozwa na Monsinyo Krzysztof Josef Nykiel, Hakimu wa Idara ya Toba ya Kitume. Saa 5.00 asubuhi katika Uwanja wa Madhabahu ya Bikira Maria wa Loreto itafutia afla fupi kuanza na  Wimbo wa Taifa la Vatican na wa Italia kabla ya kusoma  Tamko rasimi  la kuanza Jibilei ya Mama Maria na baadaye  itafuata sala ya Malaika wa Bwana. Mwaka mtakatifu wa Jubilei ya Mama Maria, itaanza kunako tarehe 8 Desemba na kumalizika tarehe 10 Desemba 2020.

31 October 2019, 12:08