Tafuta

Vatican News
Nembo  mbiri zinazoongoza ziara ya kitume ya Papa Francisko nchini Thailand na Japan Nembo mbiri zinazoongoza ziara ya kitume ya Papa Francisko nchini Thailand na Japan 

Ratiba ya Hija ya Kitume ya Baba Mtakatifu kwenda nchini Thailand na Japan imetolewa!

Tarehe 2 Oktoba imetangazwa ratiba ya Ziara ya Kitume ya Baba Mtakatifu Francisko ya kwenda nchini Thailand na Japan inayotarajiwa kuanza tarehe 19 hadi 26 Novemba 2019. Katika ziara hiyo Baba Mtakatifu anaongozwa na kauli mbiu ya "wafuasi wa Kristo ni wafuasi wa kimisionari” na nchini Japan anaongozwa na kauli mbiu ya kulinda maisha yote.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ziara ya Kitume ya Baba Mtakatifu Francisko ya kwenda nchini Thailand  na Japan  iliyotangazwa tarehe 13 Septemba 2019 , itazna tarehe 19 katika uwanja wa Fiumicino kuelekea Thailand na ndiyo hatua ya kwanza na kufika kesho. Atabaki nchini humo hadi tarehe 23 Novemba. Kauli mbiu ya ziara ya kitume nchini humo ni “ wafuasi wa Kristo ni wafuasi wa kimisionari” moto inayoangazia maadhimisho ya miaka 350 tangu kuanzishwa Makao ya Kitume ya Vatican  huko Siam kunako mwaka 1669.

Mara baada  ya kukaribishwa na gwaride la Kijeshi katika  uwanja wa ndege wa Bangkok, Baba Mtakatifu atakwenda kwenye nyumba ya rais ambapo katika uwanja kutakuwapoa na afla ya kumkaribisha. Katika ukumbi watakutana na waziri Mkuu na baada ya kwenda katika ukumbi wa mkutano na kutoa hotuba yake kwa viongozi wa ngazi zote na wa kidiplomasia.  Siku zitakazo fuata itakuwa ni kufanya mikutano na watu wa Mungu nchini humo kama kawaida ya ziara nyingine za kitume.

Ziara nchini Japan

Baada ya afla za kuwaagwa katika uwanja wa ndege huko  Bankok, Jumamosi tarehe 23 Novemba 2019 Baba Mtakatifu atakwenda Nchini Japan ambapo atakaa huko hadi Jumanne tarehe 26 Novemba. Kauli mbiu inayoongoza ziara yake ya kitume ni “ Kulinda maisha yote” ambayo  katika nemba inaonesha ishara ya msalaba na ambayo imetolea katika sala ya wakristo kuhusiana na kazi ya uumbaji ambayo inahitimisha Wosia wa Kitume wa Baba Mtakatifu wa Laudato Si.

Ujumbe  kuhusu silaha za kinyuklia

Baba Mtakatifu Francisko anatarajia kufika mjini Tokio -Haneda majira ya saa 11.40 masaa ya Ulaya. Siku ya kwanza itakuwa ni kukutana na maaskofu katika ubalozi  wa Vatican nchini humo na kutoa hotuba yake. Jumapili atatembelea Nagasaki na Hiroshima.  Katika mji wa kwanza ambao atafika  na ndege kutoka Tokyo kutakuwepo na ujumbe wake “kuhusu silaha za kinyuklia katika uwanja wa kituo cha bomu la kinyuklia na ambapo atatoa  pia heshima kwa watakatifu wafiadini katika jumba la makumbusho ya wafiadini la Nishizaka Hill, kwa sala zake na kusali sala ya Malaika wa Bwana. Baada ya chakula cha mchana katika  nyumba ya Askofu Mkuu itafuata Misa Takatifu katika uwanja  wa michezo. Na baadaye Baba Mtakatifu anatarajia  kwenda na ndege huko Hiroshima, mahali atatoa ujumbe wake katika mkutano kwa ajili ya amani. Na jioni atarudi jijini Tokyo.

02 October 2019, 14:49