Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu mkuu Bernardito Cleopas Auza kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Hispania na Andorra. Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu mkuu Bernardito Cleopas Auza kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Hispania na Andorra. 

Askofu mkuu Auza ateuliwa kuwa Balozi Hispania na Andorra

Askofu mkuu Auza alizaliwa mwaka 1959 huko Tallibon, nchini Ufilippini. Akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 29 Juni 1985. Tarehe 8 Mei 2008 akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini Haiti na kuwekwa wakfu kuwa Askofu mkuu, tarehe 3 Julai 2008 na Kardinali Tarcisio Bertone, aliyekuwa Katibu mkuu wa Vatican kwa wakati ule.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Bernardito Cleopas Auza kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Hispania na Andorra, moja ya nchi ndogo sana duniani. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Auza alikuwa ni Mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, nchini Marekani.

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Bernardito Cleopas Auza alizaliwa kunako tarehe 10 Juni 1959 huko Tallibon, nchini Ufilippini. Baada ya kuhitimu masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 29 Juni 1985 na Askofu Daniel Francis Walsh. Tarehe 8 Mei 2008 akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini Haiti. Akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu hapo tarehe 3 Julai 2008 na Kardinali Tarcisio Bertone, aliyekuwa Katibu mkuu wa Vatican kwa wakati ule.

02 October 2019, 06:53