Vatican News
Baba Mtakatifu amemteua Mheshimia Padre  Moses Chikwe wa Jimbo Kuu Katoliki la Owerri nchini Nigeria, kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Baba Mtakatifu amemteua Mheshimia Padre Moses Chikwe wa Jimbo Kuu Katoliki la Owerri nchini Nigeria, kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu   (ANSA)

Padre Moses Chikwe ameteuliwa kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Owerri-Nigeria

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Moses Chikwe wa Jimbo Kuu Katoliki la Owerri nchini Nigeria,kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu hilo.Hadi uteuzi huo Askofu mteule alikuwa ni Mkurugenzi wa Elimu Jimbo Kuu katoliki la Owerri na kushirikiana na Parokia ya Mtakatifu Thomas More Jimbo Kuu hilo.

Vatican news- Vatican 

Alhamisi tarehe 17 Oktoba 2019, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Moses Chikwe wa Jimbo Kuu Katoliki la Owerri nchini Nigeria, kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Kuu hilo. Hadi uteuzi wake, Askofu mteule alikuwa ni Mkurugenzi wa Elimu Jimbo Kuu katoliki la Owerri na akishirikiana na Parokia ya Mtakatifu Thomas More Jimbo Kuu Katoliki la Owerri Nigeria na mbaye amepewa makao ya Flumenzer.

Askofu Mteule msaidizi wa jimbo kuu Katoliki la  Owerri, Padre Moses Chikwe alizaliwa tarehe 4 Aprili 1967 huko Uzoagba-Ikeduru, Jimbo Kuu Katoliki la Owerri.  Majiundo yake  ya kifalsafa ni katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Joseph huko Ikot-Ekpene (1988-1992), ikifuatia Taalimungu katika Seminari Kuu ya Bigard, Enugu Nigeria (1992-1996. Kunako  mwaka 2013 alikamilisha shahada ya Udaktari  wa Elimu ya usimamizi katika Chuo Kikuu cha California huko Los Angeles, Marekani. Padre Chikwe alipata daraja la upadre  kunako tarehe 6 Julai 1996 katika Jimbo Kuu Katoliki la Owerri. Na tangu wakati huo ameweza kufunika nafasi mbalimbali za utume kwenye ofisi za Jimbo Kuu la Owerri, Nigeria.

17 October 2019, 12:05