Tarehe 17 Oktoba 2019 majira ya jioni, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na watu asilia wanaoshiriki Sinodi ya Maaskofu kuhusu Amazonia inyaoendelea Vatican Tarehe 17 Oktoba 2019 majira ya jioni, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na watu asilia wanaoshiriki Sinodi ya Maaskofu kuhusu Amazonia inyaoendelea Vatican 

Baba Mtakatifu amekutana na watu asilia na kuwaambia kuwa Injili itamadunishwe!

Tarehe 17 Oktoba 2019,mchana Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kikundi cha watu asilia wanaoudhuria Sinodi kuhusu Amazonia inayoendelea wakati huu.Ni kwa mujibu wa habari kutoka kwa msemaji mkuu wa Vyombo vya habari Vatican Dk. Matteo Bruni.Amekazia juu ya kutangaza Injili katika kila kona kulingana na lugha na utamaduni mahalia.

Tarehe 17 Oktoba, saa 9.30 alasiri, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kikundi karibia cha watu arobaini wa asilia ambao ni kati ya washiriki wa Sinodi kwa ajili ya Kanda ya Amazonia inayoendelea mwezi huu na shughuli nyingine zilizoanzishwa hapa Roma kwa siku hizi. Aliyewasindikiza watu hawa ni Askofu Mkuu Roque Paloschi wa Jimbo Kuu Katoliki la  Porto Velho,  na Kardinali Claudio Hummes.

Kwa mujibu wa msemaji mkuu wa Vyombo vya habari Vatican, Dk Bruni anasema mkutano umefunguliwa kwa hotuba fupi kutoka  sauti mbili, moja imesomwa na mwanamke na nyingine mwanaume, wawakilishi wa watu asilia na ambao wemeweza kutoa shukrani kubwa kwa Baba Mtakatifu Francisko  kwa ajili ya kuitisha Sinodi na kumwomba msaada wa kuendeleza shauku yao, hasa ya kuhakikisha utulivu wa maisha na furaha ya watu wao, huku wakitunzwa katika ardhi yao, kulinda maji na ili  waweze kweli kufurahia urithi wa mababu zao.

Naye Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya kuwasikiliza ametoa baadhi ya tafakari yake kwa wawakilishi hao, akisisitiza kwa jinsi gani Injili ni kama mbegu inayoanguka katika kila ardhi yoyote na kukua kulingana na aina ya udongo huo. Akigusaia juu ya Kanda ya Amazonia, Baba Mtakatifu Francisko amebainisha juu ya hatari za mitindo mipya unayoibuka ya ukoloni. Na hatimaye akigusia juu ya  chimbuko la Ukristo, uliozaliwa katika dunia ya kiyahudi na kukua katika dunia ya kigiriki-Kilatino, hadi kufikia hata ardhi nyingine, kama vile mashariki, magharibi na Amerika, Baba Mtakatifu Francisko amesisitizia umuhimu wa  Injili kutamadunishwa kwani amesema kuwa, watu wanapokea Habari Njema ya Yesu kupitia utamaduni wao.

18 October 2019, 09:50