Tafuta

Vatican News
Dk. Jean -Marie Montel  ameteuliwa kuwa mshauri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican Dk. Jean -Marie Montel ameteuliwa kuwa mshauri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican  

Dk. Montel ametuliwa kuwa mshauri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano

Dk. Jean-Marie Montel kutoka nchini Ufaransa anashikilia nafasi ya naibu mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Wahariri ya Bayard pia ni Rais wa Shirikisho la Vyombo vya Habari Katoliki nchini Ufaransa.Kwa sasa ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa mshauri mpya wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ili kuendeleza jitihada za Kanisa katika mchakato wa uinjilishaji kwa njia za kisasa zaidi.

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko  amemteua Dk. Jean-Marie Montel, kuwa mshauri katika Baraza la Kipapa la Mawasiliano. Dk. Jean-­Marie Montel ni mkurugenzi mkuu msaidizi wa Bodi ya wahariri ya Bayard na Rais wa Shirikisho la Vyombo vya Habari katoliki nchini Ufaransa.

Wasifu wa Dk. Jean-Marie Montel

Dk.  Jean­-Marie Montel ni mwenye shahada katika Taasisi ya Mafunzo ya kisasa huko Grenoble na Taasisi ya Habari nchini Ufaransa. Katika maisha yake amewahi kushika majukumu mengi katika nyanja za kikanisa, vyombo vya habari na vyama vya mbalimbali kama vile kuwa: mwakilishi wa mawasiliano kwa ajili ya Chama cha Scout cha Ufaransa kuanzia 1995 - 2001; mwakilishi mkuu wa Chama cha Civisme et Démocratie tangu 2001 - 2005; rais na mkurugenzi mkuu wa Malesherbes Publications (Bodi ya wahariri wa La Vie-Le Monde) tangu mwaka 2006 – 2012; Mkurugenzi mkuu wa Gazeti la Milan tangu mwaka  2012 - 2013, kabla ya kuingia kufanya sehemu ya Bodi ya Bayard kunako 2013.

Tangu Julai 2017 amekuwa ni naibu Mkurugenzi mkuu wa kikundi hicho cha mwisho cha waandishi wa habari kinachounganisha Shirika moja liitwalo "Assunzionisti" na ambapo pamoja na mambo mengine wanachapisha na gazeti kila siku liitwalo “ La Croix”. Kadhalika Dk.Jean-Marie Montel ni Rais wa “Via Aeterna”,  ambalo ni tamasha la muziki la  Mont Saint-Michel na  katika eneo lake.

Toleo la Siku za Kimataifa za Mtakatifu Francis wa Sales

Hata hivyo kama Rais wa Shirikisho la Vyombo vya Habari Katoliki nchini Ufaransa, tangu Januari 2018, kwa kushirikiana na Baraza la Kipapa la Mawasiliano, wameweza kuandaa Siku za Kimataifa za Mtakatifu Francisko wa Sales na ambapo  toleo lingine lijalo litafanyika huko Lourdes kuanzia  tarehe 22 hadi 24 Januari 2020.

30 October 2019, 14:46