Tafuta

Starehe 28 Oktoba 2019 imetiwa sahihi ya pamoja  katika Hati kuhusu mwisho wa maisha Starehe 28 Oktoba 2019 imetiwa sahihi ya pamoja katika Hati kuhusu mwisho wa maisha 

Hati ya Dini za Ibrahimu:hakuna kifo laini!

Katika Hati ya pamoja ya Dini za Kiibrahimu inayohusu matatizo ya kifo,inataka kuhakikisha kwamba mapenzi ya mgonjwa yasitazamwe kama mzigo kwa upande wa kifedha hadi kumfikisha achague kifo,badala yake apatiwe tiba na msaada wa kusindikizwa hadi mwisho wa maisha yake.Dini za Kiibrahimu zinachukulia kujiua ni dhambi kwa sababu maisha ni matakatifu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika Hati ya pamoja ya Dini za Kiibrahimu inayohusu matatizo kifo, ambayo imetangazwa tarehe 28 Oktoba 2019, inaonesha kupinga kila aina ya eutanasia na kama ilivyo hata njia zozote za wasindikiza kifo laini kwa sababu ni matendo ambayo yanakwenda kinyume na thamani ya maisha ya mwanadamu na matokeo yake ni makosa kwa mtazamo wa maadili kidini na inapaswa isitishwe bila masharti. Jamii lazima zihakikishe inakuwapo tiba ya mgonjwa na hatimaye bila kutazama mgonjwa kama mzigo kwa upande wa kifedha ambapo umepelekea mgonjwa kuwa na uchaguzi mbaya na kwa maana yake ni vizuri mgonjwa akaweza kusindikizwa ili kuishi kwa kipindi kinachobaki kwa kusaidiwa na kwa utulivu.

Nafasi ya dini za ibarahimu kuhusu mwisho wa maisha

Kuna hatua mbalimbali zinazooneshawa katika Hati  ya pamoja ya dini za Kiibrahimu kuhusiana na mwisho wa maisha, chini ya usimamizi na ushirikiano na Vatican. Maandishi ya Hati hiyo yanalenga kuwasilisha msimamo wa dini zote zenye imani moja ya Ibarahimu juu ya maadili na mazoezi yanayofaa kwa wagonjwa walio katika hatua ya mwisho wa maisha yao kwa faida ya wagonjwa hao, wanafamilia, wataalamu wa afya na viongozi wa kisiasa wanaoshikilia moja ya dini hizi.  Lakini pia kuboresha uwezo wa wataalamu wa afya katika kuelewa, kusaidia na kufariji mwamini  na familia yake wakati wa kipindi cha mwisho wa maisha na pia kukuza uelewa na uhusiano kati ya njia tofauti za kidini na utamaduni wa dini zote za kiibrahimu ( Wakristo, Wayahudi na Waislamu) na maadili ya kidunia kuhusu imani, maadili, vitendo vinavyohusiana na mgonjwa katika hatua hiyo ya mwisho wa maisha yake.

Teknolojia inarefusha maisha, lakini mara nyingi kwa uchungu na mateso

Katika utangulizi Hati hiyo inasisitiza kuwa maswala yanayohusu maamuzi ya mwisho wa maisha yanatokea shida ambazo siyo rahisi, na zinazoongezewa na maendeleo ya hivi karibuni, kama  vile maendeleo makubwa ya kisayansi na kiteknolojia na  ambayo yanawezekana kuongezea maisha katika hali na njia ambazo hadi sasa zilikuwa hazijafikiriwa. Kwa bahati mbaya kuishi kwa muda mrefu mara nyingi usindikizwa na mateso na maumivu kwa sababu ya hali mabadiliko ya viungo, akili na hisia. Uhusiano wa daktari na mgonjwa umebadilika kwa maana uhusiano huo siyo tena  wa kibaba, bali umekuwa wa kujitegemea na uhuru kwa kiasi kikubwa.  Na uhuru huo umepelekea mambo mengi kwa mfano, watu katika nchi zilizoendelea wanakufa katika mahospitali au zahanati na katika mazingira yasiyo ya mtu  binafsi  au yasiyokuwa ya kawaida, wakati wa nyakati zilizopita, watu walikuwa wanafia nyumbani wakiwa wamezungukwa na wapendwa wao katika mazingira yanayojulikana na ya kawaida. Aidha pia kuna ushiriki mkubwa wa wataalamu tofauti katika matibabu ya wagonjwa kwenye awamu ya mwisho katika mitandao, mfumo wa mahakama na maoni ya umma. Na mwishowe,kila wakati kuna rasilimali za kubeba matibabu ya gharama kubwa.

Maamuzi kuhusu wagonjwana huruma kuelekea kwa anayekufa

Katika Hati hiyo inaeleza wagonjwa ambao wako karibu na mwisho wao, kutokana na ugojwa usiotibiwa na asili yake siyo ya kidaktari-kisayansi, bali ni kijamii, kimaadili, sheria za kidini na utamaduni. Hata hivyo kanuni na mazoea ya dini za kiibrahimu siyo wakati wote zinaambatana na maadili na mazoea ya kibinadamu ya kidunia. Kutokana na hiyo inaonesha kwamba ni muhimu kuwa na huruma kwa wale wanaokufa. Je! ni muhimu kwa nani? Yote hayo yamewekwa ili kusaidia wale ambao wanakaribia kufa wakati hakuna matibabu inawezekana na  ambayo inawakilisha njia ya utunzaji wa zawadi ya uhai ya Mungu na ni ishara ya jukumu la kibinadamu na la kimaadili kwa wale ambao kufa. Njia ya jumla inahitajika na ambayo ni huruma. Kuhisi huruma na taaluma ya  kila mtu anayehusika kusaidia mgonjwa, hasa wale ambao wana jukumu la ustawi wake wa kisaikolojia na kihisi ni muhimu.

Kukataa matibabu, ikiwa kifo kinakaribia na kutoa msaada wakati wa kuandaa kifo

Katika Hati pia inaelezewa kuwa, uingiliaji wa kiafya kupitia matibabu na matibabu ya teknologia huhesabiwa kuwa haki kwa suala la msaada unaowezekana na  ambao unaweza kutolewa. Kwa sababu hiyo, matumizi yake lazima yatathminiwe ili kuhakikisha ikiwa matibabu yanasaidia au kuongeza muda wa maisha yanafikia lengo na wakati amekwishafika mipaka yake. Kwa maana hiyo wakati kifo kinakaribia licha ya njia inayotumiwa, inahesabiwa kuchukua uamuzi wa kukataa matibabu ambayo hayatafanya chochote isipokuwa kuongeza maisha magumu, mazito, na mateso. Lakini hata wakati wa kuendelea kujaribu kuzuia kifo sasa ambacho kinaonekana wazi ni vigumu kuwaza na ambapo inahitajika kufanya kile kinachowezekana ili kutoa misaada wa kupunguza maumivu, kusindikiza na msaada wa kihisia, wa kiroho kwa mgonjwa na familia yake katika maandalizi ya kifo, kwa mujibu wa Hati hiyo.

Kuheshimu mapenzi ya anayekufa ambaye anataka kuongeza maisha:zuia kifo laini

Katika  Hati  inathibitisha kwamba Madaktari na jamii, wanapaswa kuheshimu mapenzi  halisi ya mgonjwa anayekufa na ambaye anataka kuongeza muda na kuokoa maisha yake hata ikiwa ni kwa kipindi kifupi tu, kwa kutumia matibabu sahihi. Mapenzi hayo yanaamanisha mwendelezo wa usaidizi wa kupumua, lishe ya bandia na uhamishaji wa maji, kwa njia ya maelekezo ya moja kwa moja au kwa njia ya jamaa yake wa karibu. Katika kesi ya mgonjwa mwamini au kama jamaa ni mwamini, padre au mtu yoyote wa dini anaweza kushauri. Kwa kifupi, Hati hiyo inazungumzia pia  juu ya maswali yanayohusu muda na maana ya maisha ya mwanadamu hambayo ayapaswi kuwa uwanja wa wafanyia kazi mazoezi ya afya na kwamba ni  jukumu la kutoa huduma bora na msaada wa hali ya juu kwa aliye wagonjwa. Kwa maana hiyo, dini za  kiibrahimu zinapinga aina yoyote ya eutanasia, ambayo ni hatua ya moja kwa moja ya kukusudia kuondoa maisha na vile vile hata msaada wa kujiua ambao ni msaada wa moja kwa moja wa makusudi, na  kwa sababu ni vitendo ambavyo vinakwenda kinyume kabisa na thamani ya maisha ya mwanadamu na kwa hivyo vitendo vibaya kwa mtazamo wa maadili na kidini vinapaswa kukatazwa bila masharti..

Kusaidia mgonjwa asihisi uzito kiuchumi

Kwa msaada wa jumuiya ya mgonjwa aliye hatua ya mwisho wa maisha yake na familia yake, katika maamuzi ambayo anapaswa anakabiliane naye, katika Hati inaonesha uwepo na sasisho la muundo na taasisi kupitia msaada wa afya na dini. Kwa hakika  jamii lazima ihakikishe kuwa mapenzi  ya mgonjwa  yasiwe kama mzigo kwa mtazamo wa kifedha na kumpelekea mgonjwa achague kifo badala ya kutaka matunzo na msaada unaomwezesha  kuishi muda unaobaki kwa faraja na utulivu. Na wakati huo huo Hati hiyo inashauri wagonjwa ambao ni waamini na kwa familia zao, kama msaada wa wa kijumuiya kuwa na kipindi cha sala na tafakari na msaada wa madakatari na watu wa dini.  Ni msaada ambao ni  jukumu la kila jamuiya ya imani iliyo nayo kwa washiriki wake.

Kuhakikisha msaada wa kiroho na wa kidini kwa wale wanaokufa

Hata hivyo Hati  pia mejikita kuelezea juu ya msaada wa kiroho na kidini, unaofafanuliwa kama njia ya haki msingi kwa mgonjwa na jukumu la jumuiya ya kidini na mchangowa wa ubinadamu katika  kifo. Wahudumu wote wa afya wanahitaji kuunda hali ambayo msaada wa kidini umehakikishwa kwa mtu yeyote anayeomba, kwa uwazi au kwa njia nyingine.

28 October 2019, 13:30