Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Rais wa Baraza la Ulaya Bwana Donald Tusk Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Rais wa Baraza la Ulaya Bwana Donald Tusk  (ANSA)

Papa Francisko amekutana na Bw.Tusk,Rais wa Baraza la Ulaya!

Katika nyumba ya Kitume mjini Vatican, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Rais wa Baraza la Ulaya Bwana, Donald Tusk na baadaye amekutana na Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin.

Tarehe 5 Oktoba 2019, Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican na rais  wa Baraza la Ulaya Bwana Donald Tusk, ambaye baada ya mkutano huo amekutana pia na  Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin.  Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa vyombo vya habari Vatican kuhusiana na mkutano huo.

Katika harakati za mazungumzo yao viongzo hawa wameonesha uhusiano mwema uliopo kati sehenu zote mbili ikiwa ni pamoja na kutazama mchango wa Kanisa unaotolewa na mapenzi ya kutaka kuendelea kujikita nao kwa ajili ya ujenzi wa Ulaya ya mshikamano, amani na heshima ya utambulisho wa watu wote waliomo. Aidha katika majadiliano yao, pia wamesisistiza juu ya baadhi ya masuala yenye tabia ya kimataifa na kikanda, kwa namna ya pekee kama vile umakini wa umoja wa Ulaya kwa wale wanaotaka kujiunga na Umoja wa Ulaya na uhamiaji.

 

05 October 2019, 15:31