Tafuta

Vatican News
Askofu Vincenzo Paglia akihutubia wakati wa uwasilishaji wa Hati kuhusu Mwisho wa Maisha Jumatatu tarehe 28 Oktoba 2019 Askofu Vincenzo Paglia akihutubia wakati wa uwasilishaji wa Hati kuhusu Mwisho wa Maisha Jumatatu tarehe 28 Oktoba 2019 

Askofu Paglia:msisababishe vifo kwa wagonjwa!

Wawakilishi wa dini za Kiibrahim yaani Wakristo,Wayahuidi na Waislamu wametia sahihi tarehe 28 Oktoba mjini Vatican katika Hati ya pamoja juu ya Mwisho wa Maisha huku wakikataa kabisa juu ya matendo ya kifo laini na wakati huo huo,wanaungana pamoja kujikita kwa jitihada zote katika kulinda maisha hadi kufikia kifo cha kawaida.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 28 Oktoba 2019 umefanyika mkutano kwa ajili ya kuwakilisha Hati ya pamoja na kutia sahihi kwa Hati inayohusu hatua ya mwisho ya kifo na ambapo katika  salam za Askofu Vincenzo Paglia Rais wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya maisha na Kansela wa Taasisi ya Kipapa ya Ndoa na Familia ya Yohane Paulo II, amewasalimu Wawakilishi wa dini za Kiibrahim(wakristo,wahayahudi na waislamu) na kutia sahini ya pamoja katika mada hiyo nyeti kwenye  kipindi hiki cha kihistoria.  Askofu Paglia amesema kuna mambo matatu msingi ambayo anafikiri ni muhimu kwa kipindi hiki. Kwanza kiini cha mada ambayo wote wanafahamu  yaani kuhusu  vitendo vya kifo laini katika mantiki ya jamii ya sasa. Mjadala huo haufanyiki ndani ya jumuiya ya kisayansi  na katika  mada kwa lengo la  rasilimali za tiba ambayo imewezesha madawa kufikia hatua ya mwisho huo, lakini pia ni maono mapana ya utamaduni kwa ujumla yanayohusiana na masuala hayo kuhusu kifo laini. Huo anaoneza kusema ni ufunguzi wa nafasi mpya za uchaguzi wa kutimiza; ni wajibu kwa wote katika kuchagua kwa namna ya kujenga na kukuza hadhi ya kila mtu. Hati ya pamoja ambayo  wametia sahihi, inatoa nwaliko muhimu kwa ajili ya madawa na wataalum wa afya. Madawa peke yake hayana maono ya kutoa au kuondoa maisha ya wagonjwa. Kufanya uamuzi kutoa maisha ya mtu kwa maana yake ni kukana maana ya maisha kamili ambayo tumepewa kama zawadi kutoka kwa Mungu.  Upo utambuzi ambao unajikita kwa dhati katika eneo ambalo ni gumu na  kutembea katika mambo yenye mantiki zake. Kila jamii inaalikwa kushirikana katika nyanja zote za rasilimali iwe binafsi na kijumuiya, ishara, kusimulia, sanaa na zaidi hasa  katika dini zote.

Huduma shufaa

Katika kujikita kutoa huduma shufaa (palliativu care) inasisitiza mantiki hiyo , anabainisha Askofu Paglia. Kwa maana hiyo katika Hati ya pamoja inasisitiza umuhimu wake na jitihada za kufanya kutambua nafasi yake ili kueneza kila sehemu na mazingira yoyote na ambayo ni mwafaka kama vile  vyuo vikuu. Lengo ni kujikitia katika kumtunza mtu kwa maana kila kitu yaani mfungamano kuanzia matibabu, uchungu hadi kufikia ukuu wake na kuthamanisha maono ya kiroho ambayo mtu wa kibinadamu anaishi. Pili ukuu wa kidini na kiekumene katika tukio hili ambalo kwa namna ya pekee ni pamoja na mantiki tunaomoishi ya dunia ya leo iliyogawanyika vipande vipande na maoni tofauti ya uhuru wa binadamu. Katika hili inahitaji majadilianio na uwezekano wa kupokeana kwa pamoja kama mchakato ulioanza na ambao unajiendeleza katika hati hiyo.  Aidha jambo msingi ni kufanya mazoezi binafsi na kushuhudia kwa wote, kuanzia na uwajibikaji na kushirikiana kwa ajili ya kufikia kugundua maendeleo ambayo yanaweza kuleta matunda  mengi ya pamoja. Iwapo watakuwa pamoja na kufanya kazi kwa pamoja , kwenye huduma ya wanawake na wanaume wa dunia hii na ambao ni watoto wa Mungu mmoja, ni wazi kabisa inawezekana kujitambua kwa mara nyingine kuwa ni ndugu, kaka na dada ambao wanaalikwa kuunganisha nguvu pamoja ili kutoa jibu la maswali yanayo ulizwa na wengi.

Hatua ya kujenga utamaduni wa makutano

Askofu Paglia aidha amesema jambo la  tatu muhimu kuwa  leo ni  hatua moja wapo ya kuelekeakatika  kujenga ule utamaduni wa makutano ambao Baba Mtakatifu Francisko anatufundisha  kusifu  na kufanyia mazoezi ambayo kwa namna moja, dini zote za kiibrahimu zinaweza kweli kukuza.  Na kwa njia hii wanaweza kweli kuwa na utamaduni wa majadiliano kama njia; ushirikiano wa pamoja kama mwongozo; utambuzi wa kuendeleza, kama mtindo na mantiki hii. Ni kwa mujibu wa kile kilichoandikwa kwenye Hati ya Udugu wa Kibinadamu wa Abu Dhabi. Hii siyo kazi ya kushitukiza, bali ni tunda la jitihada inayotazama awali ya yote mwendelezo wa dhamiri binafsi na ambayo inaweza kupelekea kuungana hata  latika misningi ya kitaasisi ambayo wataweza kuitambua na kuigundua. Kwa maana hiyo majadiliano ni fadhila. Si jambo la kibinafsi, bali linaloelekeza malengo na msimamo wa kukuza mtindo wa maisha ambayo yanakuza utafiti na uchaguzi wa ustawi wa dhati katika hali na mada binafsi ambazo zinatakiwa kukabiliwa. Dini za kiibrahimu zinaweza kuelewa na kwa ajili ya kujieleza kwa namna ya ushirikisho wa jitihada ambayo ndiyo iliyo kubwa zaidi. Inawezekana kutoa mchango mzito na si tu kinadharia kwa ajili ya kutafakari kwa kina maana ya maisha ya binadamu, lakini pia kimatendo, kwa njia ya kutoa huduma ya jumuiya za waamini, kwa ajili ya kushuhudia pamoja ule uwajibikaji wa kile kinachotuunganisha mmoja na mwingine.

Inahitajika uwezo wa kila mmoja,kuwapo katika mzunguko wa umma na kushirikiana

Hata hivyo Askofu Paglia amesema wanataka kupanua mwangaza wa  mawasiliano yao ambayo ni muhimu katika  ujumbe nyeti ambao wanataka waukuze. Hii ina maana ya kuweka chachu katika jamii ambamo jumuiya zote zinaishi kwa kuwashirikisha wanaume na wanawake wenye mapenzi mema na katika nafasi mbalimbali na kazi wanazojikita nazo. Inahitajika si kutafuta  tu,  lakini pia kuzalisha ubunifu wa zile fursa ambazo zinaweza kujitokeza katika hili. Kwa hakika jambo hili linahitaji uwezo wa kila mmoja, kuwapo katika mzunguko wa umma na kushirikiana katika  hotuba mbalimbali zinazoweza kueleweka kwa wale ambao katika dunia wanatafsiri vingine na katika maisha ya binadamu. Lugha ya Hati ya pamoja inajibainisha yenyewe wazi, huku ikitoa kipaumbele cha kazi hiyo na kutoa mantiki nyingi katika kusaidia uelewa. Kwa maana hiyo ni mtazamo ambao unajikita kwenye wakati endelevu na ndilo lengo la kuishi kwa siku hiyo ya mkutano huo.

28 October 2019, 13:40