Tafuta

Baba Mtakatifu amemteua Askofu mkuu Paolo Borgia kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Pwani ya Pembe. Baba Mtakatifu amemteua Askofu mkuu Paolo Borgia kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Pwani ya Pembe. 

Askofu mkuu Paolo Borgia, Balozi wa Vatican Pwani ya Pembe

Askofu mkuu Paolo Borgia alizaliwa huko Manfredonia, Foggia, nchini Italia hapo tarehe 18 Machi 1966. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa daraja Takatifu ya Upadre tarehe10 Aprili 1999. Ana shahada ya uzamivu katika Sheria za Kanisa. Tarehe 1 Desemba 2001 alijiunga na utume wa Kidiplomasia mjini Vatican na tangu wakati huo, ametumwa sehemu mbali mbali za dunia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Paolo Borgia kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Pwani ya Pembe, Ivory Coast. Kabla ya uteuzi huu alikuwa ni Afisa mwandamizi aliyekuwa anashughulikia masuala ya jumla kwenye Sekretarieti kuu ya Vatican. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Borgia aliwekwa wakfu na Baba Mtakatifu Francisko hapo tarehe 4 Oktoba 2019, kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Askofu mkuu Paolo Borgia alizaliwa huko Manfredonia, Foggia, nchini Italia hapo tarehe 18 Machi 1966. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa daraja Takatifu ya Upadre tarehe10 Aprili 1999. Ana shahada ya uzamivu katika Sheria za Kanisa.

Tarehe 1 Desemba 2001 alijiunga na utume wa Kidiplomasia mjini Vatican na tangu wakati huo, ametekeleza utume wake huko Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati, Mexico, Israel na Lebanon. Baadaye alibadilishiwa utume na kupelekwa kwenye kitengo cha mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican na mwishoni, tarehe 4 machi 2016 aliteuliwa kuwa afisa mwandamizi aliyekuwa anashughulikia masuala ya jumla katika Sekretari kuu ya Vatican.

Pwani ya Pembe
29 October 2019, 11:00