Tafuta

Vatican News
Papa Francisko amemteua Askofu mkuu Joseph Salvador Marino kuwa Rais mpya wa Taasisi za Kipapa Kikanisa. Papa Francisko amemteua Askofu mkuu Joseph Salvador Marino kuwa Rais mpya wa Taasisi za Kipapa Kikanisa.  (ANSA)

Askofu mkuu Joseph Marino, Rais wa Taasisi za Kikanisa

Askofu mkuu Joseph Salvador Marino alizaliwa mwaka 1953. Akapewa Daraja Takatifu la Upadre mwaka 1979. Akaanza utume wa diplomasia ya Kanisa mwaka 1988. Tarehe 12 Januari 2008, akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Balozi wa Vatican nchini Bangaladesh na kusimikwa kuwa Askofu mkuu tarehe 29 Machi 2008.. Ametumikia: Malaysia, Timor M. na Brunei.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Joseph Salvador Marino kuwa Rais wa Taasisi za Kipapa Kikanisa. Kabla ya uteuzi huu Askofu mkuu Marino alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Malaysia, Timor ya Mashariki na Brunei. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Joseph Salvador Marino alizaliwa tarehe 23 Januari 1953 huko Birmingham, nchini Uingereza. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja Takatifu la Upadre hapo tarehe 25 Agosti 1979. Alianza utume wa diplomasia ya Kanisa mjini Vatican, tarehe 15 Julai 1988. Na tangu wakati huo, amewahi kufanya kazi huko nchini Ufilippini, Uruguay, Nigeria, Vatican pamoja na Uingereza.

Tarehe 12 Januari 2008, akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Balozi wa Vatican nchini Bangaladesh na kusimikwa kuwa Askofu mkuu tarehe 29 Machi 2008. Tarehe 16 Januari 2013, akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Balozi wa Vatican nchini Malaysia, Timor ya Mashariki na Mwakilishi wa Kitume nchini Brunei. Tarehe 11 Oktoba 2019, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Rais wa Taasisi za Kipapa Kikanisa.

Taasisi za Kikanisa
12 October 2019, 14:52